Wednesday , 8 May 2024
Home Kitengo Maisha Burudika Wizkid, Burnaboy wan’gara tuzo za grammy, Beyonce aweka rekodi
BurudikaTangulizi

Wizkid, Burnaboy wan’gara tuzo za grammy, Beyonce aweka rekodi

Spread the love

 

TUZO kubwa ulimwenguni, zinazotolewa nchini Marekani maarufu ‘Grammy,’ zimeshuhudia gwiji wa muziki, Beyonce akiweka rekodi kwa kushinda na kufikisha tuzo 28 tangu kuanzishwa kwake huku wasanii, Burna Boy na Wizkid, wakiwakilisha vyema bara la Afrika. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Tuzo hizo, zimetolewa usiku wa kumkia leo Jumatatu, tarehe 15 Machi 2021, ambapo wasanii mbalimbali wa Marekani wameendelea kuvunja rekodi na kung’ara zaidi.

Beyonce amekuwa mwanamke wa kwanza duniani, kufikiza idadi hiyo ya tuzo zenye thamani kubwa duniani huku Burna Boy pomoja na Wizikid, wote kutoka nchini Nigeria nao wakijinyakulia tuzo.

Burna Boy ameshinda kipengele cha albamu bora ya muziki ulimwenguni inayoitwa ‘Twice as tall’ na Wizikid amefanikiwa kushinda kipengele cha video bora ya wimbo wa ‘brown skingirl’ alioshirikishwa na Beyonce.

Pia, Blue Ivy, mtoto wa Beyonce, amefanikiwa kushinda tuzo katika wimbo huo wa Brown Skin girl kwa kushiriki vema kwenye video hiyo.

Katika kipengele cha video bora, tuzo hutolewa kwa msanii, muongoza video pamoja na mtayarisha wa video husika iliyoshinda.

Mwaka 2021, hakukuwa na watazamaji wa moja kwa moja na watumbuizaji walikuwa wametenganishwa kwenye majukwaa matano huku wakitengana kwa umbali, ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19).

Burnaboy, ambaye jina lake halisi ni Damini Ogulu, amewahi kishiriki tuzo hizo mwaka 2020 lakini hakufanikiwa kushinda na mwaka huu, amewashinda washiriki wenzike wanne akiwemo Tinariwen.

Album iliyompa tuzo hiyo, imeelezwa na waandaaji wa tuzo kuwa imetengenezwa kwa viwango vya juu zaidi ulimwenguni na imekuwa fundisho kwa wasanii wengine hususan kutoka Afrika.

Katika albamu hiyo, Burnaboy amewashirikisha wanamuziki wengi duniani wakiwemo Stormzy, Youssou, Ndour, Naughty by nature, Ma chris Martin wa Coldplay na vilevile Sean Combs akiwa muandaaji mkuu.

Video ambayo imemfanya Wizikid kushinda, imeelezwa kuwa imezingatia mitindo na kusheherekea urembo wa mwanamke mweusi mahali popote duniani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CCM yaitaka TAKUKURU kuichunguza Chadema tuhuma alizoibua Lissu

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana...

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

Habari za SiasaTangulizi

Kinana: Hatukubali kushutumiwa kwa uongo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana amesema viongozi wa...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

error: Content is protected !!