Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Kesi ya Kambole kufutwa uwakili yapigwa kalenda
Habari MchanganyikoTangulizi

Kesi ya Kambole kufutwa uwakili yapigwa kalenda

Spread the love

 

KESI ya Wakili Jebra Kambole na mwenzake Edson Kilatu kufutiwa uwakili, iliyopangwa kusikilizwa leo Jumatatu tarehe 15 Machi 2021, katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imeaghirishwa hadi 19 Machi 2021. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Kesi hiyo iliyofunguliwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), dhidi ya Wakili Kambole na Edson Kilatu, tarehe 8 Oktoba 2020, ilipangwa kusikilizwa na Kamati ya Maadili ya Mawakili leo Jumatatu katika mahakama hiyo, lakini akidi haikutimia.

Katika kesi hiyo, AG anamtuhumu Wakili Kambole na Wakili Kilatu kwamba walidharau mahakama pamoja na kukiuka maadili ya taaluma ya sheria.

Na kwamba AG, alipeleka mashtaka hayo kwenye Kamati ya Maadili ya Mawakili, akiiomba itamke kuwa mawakili hao wamekiuka maadili ya taaluma ya sheria, hivyo wafutiwe uwakili.

Katika kesi hiyo, Wakili Kambole anatuhumiwa kuidharau mahakama kwa kuchapisha maudhui katika ukurasa wake wa twitter kuwa ‘Kisutu Revenue Authority’ (Mamlaka ya Mapato Kisutu).

Mahakama Kuu ya Tanzania

Wakili Kambole anadaiwa kuchapisha maneno hayo baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuwahukumu viongozi tisa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kulipa faini ya Sh. 350 milioni tarehe 10 Machi 2020.

Ni katika kesi namba 112 /2018, ambapo viongozi hao walikutwa na hatia ya makosa 12 ikiwemo kufanya maandamano yasiyokuwa na kibali mwaka 2018.

Wakili Kilatu anatuhumiwa kuchapisha maoni kwenye ukurasa wake wa facebook tarehe 08 Agosti 2020, maoni ambayo yanadaiwa ni ya kuikosoa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, kutoiheshimu mahakama hiyo, sheria na taaluma ya sheria.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awataka wahariri kufanya kazi bila uoga, upendeleo

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wahariri wa vyombo...

Habari Mchanganyiko

STAMICO yasaini mkataba wa bilioni 55.2 kuchoronga miamba GGML

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kufanya vizuri katika...

Habari Mchanganyiko

NMB yatoa traksuti za Mwenge wa Uhuru Mtwara

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa traksuti kwa mkoa wa Mtwara ambako...

Habari Mchanganyiko

Yara yaja na bima ya mazao kwa wakulima

Spread the love  WAKATI serikali ikiweka mikakati mbalimbali kuimarisha sekta ya kilimo...

error: Content is protected !!