KASI ya kuenea kwa virusi vya corona (COVID-19) nchini Ureno, inatikisa taifa hilo. Inaripoti mitandao ya kimataifa… (endelea).
Serikali ya Ureno baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya, iliamuwa kuomba msaada kutoka Serikali ya Ujerumani.
Wizara ya Ulinzi ya Ujerumani imeafiki kutuma maofisa wa afya wa jeshi lake, pamoja na vifaa vya matibabu nchini Ureno ili kukabiliana na hali hiyo.
Taarifa kutoka Ureno zinaeleza, vyumba vya wagonjwa mahututi vimeelemewa baada ya kuongezeka kwa maambukizi ya virusi hivyo.
Gazeti la Ujerumani la Der Speigel, limeripoti kuwa jeshi hilo linapanga kupeleka madaktari na maofisa wa matibabu 27 Ureno, na kwamba maofisa hao watakuwepo Ureno kwa siku tatu.
Pia vitu vitakavyopelekwa Ureno kutoka Ujerumani ni pamoja na vitanda pia mashine za kusaidia kupumua.
Serikali ya Ureno imeeleza, vimebakia vitanda saba pekee ambavyo havina wagonjwa mahututi kati ya 850.
Leave a comment