Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Profesa Jay: Mimi ni mbunge nje ya Bunge, Bob Wine… 
Habari za Siasa

Profesa Jay: Mimi ni mbunge nje ya Bunge, Bob Wine… 

Spread the love

JOSEPH Haule, maarufu Profesa Jay amesema, yeye ni mbunge nje ya Bunge. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Amesema hayo leo Alhamisi tarehe 14 Januari 2021, alipokuwa akizungumza katika kipindi cha XXL cha Clouds FM alipokwenda na Stamina kutambulisha wimbo wao mpya unaoitwa ‘Baba.’

Profesa Jay alikuwa Mbunge wa Mikumi Mkoa wa Morogoro kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kati ya mwaka 2015-2020 ambapo katika uchaguzi mkuu uliopita, alishindwa kutetea nafasi yake.

Akijibu swali aliloulizwa kwa sasa yeye si mbunge, nini kinaendelea, amesema “ubunge si lazima kuwa bungeni, mbunge ni kuwawakilisha wananchi. Kwa kuwa nimewahi kuwa mbunge wa Mikumi kwa hiyo, unaweza kuendelea kuniita mbunge nje ya Bunge. Mimi ni mgodi unaotembea.”

 

Bobi Wine

Profesa Jay ambaye ni msanii wa Hip Hop amesema, anaendelea na harakati ndani ya jimbo hilo akisisitiza hata Studio ya Wanalizombe aliyoijenga Mikumi “itaendelea kuwa Mikumi” ili kuinua vipaji mbalimbali jimboni humo.

Alipoulizwa kuhusu mgombea urais wa Uganda, Robert Kyagulanyi maarufu Bob Wine  kama anamuunga mkono, Profesa Jay amesema,  “mimi nimekuwa rafiki na Bob Wine kitambo sana.”

“Tunafurahi kusikia vijana wanakwenda kwenye ngazi za maamuzi. Sisi tunamuunga mkono Bob Wine na Jose Chamilioni anagombea huko. Vijana wanapokwenda kwenye vyombo vya uamuzi ni jambo zuri,” amesema Profesa Jay.

Wananchi wa Uganda, leo Alhamisi wanapiga kura katika uchaguzi mkuu nchini humo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!