May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Uchaguzi Mkuu Uganda: Sanduku la kura laibwa

Bobi Wine

Spread the love

VITUKO vya Uchaguzi Mkuu nchini Uganda vinaanza kudhihiri, tayari sanduku moja la kura linaripotiwa kuibwa na kutokomea kusikojulikana. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Wizi wa sanduku hilo umethibitishwa na Paul Bukenya, Msemaji wa Tume ya Uchaguzi nchini humo akieleza, sanduku hilo limeibwa likiwa na kura ndani yake.

Bukenya amesema, wizi wa sanduku hilo umetokea katika eneo la Rushenyi, Ntungano ambapo ni mashariki mwa nchini na kuwa, hajulikani mtu ama watu waliohusika kwenye wizi huo.

Amesema, tayari taarifa za wizi huo zimewasilishwa kwa tume pamoja na kwa Jeshi la Polisi ambalo sasa linaendesha msako mkali.

Hata hivyo, Bukenya amesema tukio hilo ni la bahati mbaya “tukio hili ni la bahati mbaya, kwa sasa tunalishughulikia na kisha tutatoa taarifa.”

Leo tarehe 14 Januari 2021, Raia wa Uganda wanapiga kura kumchagua rais wa nchi hiyo, Rais Museveni anakabiliana na upinzani mkali kutoka kwa Robert Kyagulanyi (Bobi Wine) (38), wanamuziki wa kizazi kipya.

error: Content is protected !!