Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Magufuli kumng’oa naibu waziri aliyeshindwa kuapa
Habari za Siasa

Magufuli kumng’oa naibu waziri aliyeshindwa kuapa

Rais John Magufuli
Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli, amesema atafanya uteuzi mpya wa Naibu Waziri wa Madini baada ya aliyemteua, Francis Ndulane kushindwa kuapa. Anaripoti Brightnes Boaz, Dar es Salaam … (endelea).

Amesema hayo leo Jumatano tarehe 9 Desemba 2020, muda mchache baada ya kumaliza kuwaapisha mawaziri na naibu mawaziri, Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Rais Magufuli amesema hayo, wakati akichambua wizara moja baada ya nyingine pamoja na mawaziri na naibu wao.

“Ninawafahamu wote niliowateua, mpaka wewe uliyeshindwa kuapa. Nafikiri nitamtafuta mwingine anayejua kuapa vizuri. Tunakupongeza utaendelea kuwa mbunge na tutacheki vizuri shahada yako,” amesema Rais Magufuli.

Amesema, lazima kuwe na naibu waziri anayeweza kusoma vizuri nyaraka mbalimbali ili asije kusaini nyaraka za muhimu bila kusoma kwa umakini.

Wakati wa kiapo, Kumba alikuwa akikosea kusoma kiapo kwa kurudia rudia hali iliyomfanya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi kumpa maelekezo.

Hata hivyo, Ndulane ambaye ni Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM) hakumaliza kiapo chake kwa Balozi Kijazi kumwomba aende akampumzike kwanza ili kupisha wengine kuendelea kuapishwa.

Kwa mujibu wa wasifu wa Ndulane uliowekwa katika tovuti ya Bunge la Tanzania, inamwonyesha ana shahada ya uzamili ya uhasibu na fedha aliyoipata Chuo Kikuu cha Mzumbe kati ya mwaka 2013 hadi 2015.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!