Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Michezo JPM: Simba, Yanga zimetuchelewesha
Michezo

JPM: Simba, Yanga zimetuchelewesha

Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Magufuli amesema wakati umefika kwa timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) kuundwa bila ya kuwa na wahcezaji wanaotoka katika vikosi vya Simba na Yanga kwa kuwa klabu hizo mbili zimechelewesha katika kupiga hatua kwenye sekta hiyo ya michezo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Maneno hayo ameyasema jijini Dodoma wakati akitoa maagizo kwa waziri mpya wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa pamoja na Naibu waziri Abdalah Ulega mara baada ya zoezi la kuwaapisha.

Wakati akitoa maagizo hayo Rais Magufuli alisema kuwa haiwezekani kila tukienda kucheza tunashindwa, sasa inabidi tuwe na timu ya Taifa isiyokuwa na Simba na Yanga kwa kuwa zimetuchelesha.

“Tumekupeleka wizara ya michezo (Innocent Bashungwa) mkafanye kazi kweli, haiwezekani tunakwenda kucheza tunashindwa tu. Tunataka tukashinde na mambo ya kwenda na Simba na Yanga tu, imefika wakati tukawe na timu ya Taifa isiyokuwa na mahusiano ya Simba na Yanga,” alisema Rais Magufuli.

Rais John Magufuli

Kauli hiyo imekuja kufuatia kuwa asilimia kubwa ya wachezaji wanaoitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) wanatokea kwenye klabu za Simba na Yanga ambao wanatawala soka la Tanzania.

Kikosi kilichopita cha Taifa Stars ambacho kiliitwa na kocha Etiene Ndayilagije kilikuwa na jumla ya wachezaji 27 kati ya hao wachezaji waliotoka kwenye klabu za Simba na Yanga walikuwa 15.

Timu hiyo ambayo kwa sasa inawania kusaka tiketi ya kufuzu kwa michuano ya kombe la Mataifa Afrika inayotarajia kufanyika mwakani nchini Cameroon ambapo Taifa Stars ipo kundi J, sambamba na timu za Tunisia, Libya na Equatorial Guinea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

Michezo

TFF, Amrouche ngoma nzito

Spread the loveVIPENGELE vya mkataba wa kazi aliotia saini Kocha Mkuu wa...

error: Content is protected !!