Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Magufuli akataa kunyonga 256, wafungwe maisha
Habari za Siasa

Magufuli akataa kunyonga 256, wafungwe maisha

Kitanzi
Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli, amewapunguzia adhabu wafungwa 256  waliohukumiwa kunyongwa na kuagiza wapewe kifungo cha maisha gerezani. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Wafungwa hao ni wale waliohukumiwa kunyongwa katika uongozi wa muhula wa kwanza wa Rais Magufuli.

Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo leo Jumatano tarehe 9 Desemba 2020, katika hafla ya uapisho wa mawaziri 21 na manaibu waziri 23, iliyofanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

“Leo ni siku ya Uhuru, najua katika kipindi cha miaka mitano mpaka leo natakiwa niwe nimenyonga watu 256  waliohukumiwa kunyongwa, sijanyonga hata mmoja, na wale 256 kwa mamlaka niliyopewa, nawapunguzia kifungo cha kunyongwa,  sasa wafungwe maisha,” ameagiza Rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema “watanyongwa na wengine, sijui Jaji Mkuu (Prof. Ibrahim Juma), inawezekana huyo atakayekuja atawanyonga.”

Rais John Magufuli

Rais Magufuli amesema ameshindwa kuchukua hatua hiyo kwa kuwa hataki kuwa muuaji.

“Sababu hao waliohukumiwa kunyongwa waliua, mimi sheria iliniambia niue 256, nani mwenye dhambi zaidi huyo alioua mmoja au mimi nitakaoua 256?” amehoji Rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema “Nimeshindwa ninaomba mnisamehe kwenye hilo, kwamba mimi nitakuwa muuaji, sababu wenzangu waliua wawili, mmoja au watatu walihukumiwa kunyongwa.”

Wakati huo huo, Rais Magufuli, amewapunguzia adhabu na kuwaacha huru baadhi ya wafungwa kati ya wafungwa 3,316, waliopendekezwa kwake na Kamishna Jenerali wa Magereza.

“Wako wengine 3,316  wana makosa madogo ya wizi wa kuku, wengine walitumikia kifungo chao kwa muda mrefu.  Kwa mujibu wa mapendeko yaliyoletwa na Kamishna Jenerali wa Magereza, nimekubali kuwapunguzia adhabu zao na wengine kuachiwa kwa mujibu wa sheria,” amesema Rais Magufuli.

Kiongozi huyo wa Tanzania ameagiza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kushughulikia suala hilo.

“Wizara ya Mambo ya Ndani kasimamieni hili kwa mujibu wa sheria, hao wakafungwe maisha wakashiriki katika kufanya kazi,” amesema Rais Magufuli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!