Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa NCCR-Mageuzi yagomea wabunge viti maalumu
Habari za Siasa

NCCR-Mageuzi yagomea wabunge viti maalumu

James Mbatia, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi
Spread the love

CHAMA cha NCCR-Mageuzi nchini Tanzania kimesema, hakiko tayari kupokea nafasi za ubunge wa viti maalumu kwani kitakuwa kinachochea machafuko kwenye jamii. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Msimamo huo umetolewa leo Alhamisi tarehe 12 Novemba 2020 na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia wakati anazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Mbatia ametoa wito huo alipoulizwa na wanahabari kama chama chake kiko tayari kupokea nafasi za ubunge viti maalumu.

Amesema, NCCR-Mageuzi hakitakubali kwa kuwa itakuwa ni kinyume na sheria inayoeleza, chama kitakachofikisha asilimia tano ya kura zote za wabunge kitakuwa na nafasi ya kupata wabunge wa viti maalum.

“Kwamba sisi NCCR- Mageuzi tutapewa viti ni suala lingine na tusingependa kuwa sehemu ya machafuko, wakati tunazungumzia muafaka halafu watupe viti maalumu kinyume na sheria, hatutakubali sababu sisi ni waasisi wa mageuzi Tanzania na tusingependa mageuzi ya demokrasia yakiukwe,” amesema Mbatia.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk. Wilson Mahera

NCCR-Mageuzi kimeungana na baadhi ya vyama vingine vya siasa vya upinzani nchini Tanzania vilivyotangaza kugoma kupokea nafasi hizo, hatua ambayo ni muendelezo wa kutoyatambua matokeo ya uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020 yaliyozalisha nafasi hizo.

Vyama vilivyotangaza kutotambua matokeo hayo kwa madai kwamba mchakato wa uchaguzi ulikiuka sheria na kanuni za uchaguzi, ni ACT-Wazalendo na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama cha Wananchi (CUF).

Matokeo hayo yaliyotangwa na Tume ya Taufa ya Uchaguzi Tanzania (NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yalikipa ushindi Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi wa Urais, ubunge, uwakilishi na udiwani.

Hadi sasa chama kilichokidhi matakwa ya kisheria kupewa nafasi hizo ni Chadema, ambacho mpaka sasa kimeweka msimamo wa kutokubali uteuzi wa wabunge viti maalumu.

Kufuatia Chadema kugomea nafasi hizo, Mbatia amesema kama mamlaka husika zitagawa nafasi hizo kwa vyama vingine  itakuwa ni kinyume.

“Viti maalumu vya ubunge vinapatikana kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa na sheria hii inaeleza bayana chama kinachopata asilimia tano ya kura za wabunge ndicho chenye nafasi kupata viti maalumu kama kuna chama kimekataa huwezi kufanya kienyeji kuwapa chama kingine huko ni kutafuta machafuko katika jamii,” amesema Mbatia.

Mbatia ameishauri NEC, ZEC na Bunge kufuata sheria katika utoaji nafasi za Ubunge Viti Maalumu ili kuepusha migogoro katika jamii.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!