Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mlipuko Beirut: Vifo vyafika 137
Kimataifa

Mlipuko Beirut: Vifo vyafika 137

Spread the love

NCHI ya Bangladesh imetangaza kupeleka msaada wa chakua na dawa haraka baada ya Mji wa Beirut, Lebanon kukumbwa na janga la mlipuko. Inaripoti itandao ya kimataifa…(endelea).

Mlipuko huo uliotokea Jumane ya tarehe 4 Agosti 2020, umesababisha vifo vya watu 137 mpaka sasa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Bangladesh Abdul Momen akitoa salamu za pole kwa wakazi wa Beirut, amesema taifa hilo linasikitishwa na vifo vilivyotokana na mlipuko huo.

Mlipuko huo uliosababishwa na tani 2750 za sumu ya Amonium Nitrate ziliokuwa imehifadhiwa katika ghala moja kwenye bandari ya mji huo, pia umesababisha majeraha kwa watu zaidi ya 4000.

Sumu hiyo imeripotiwa kuwa katika ghala hilo mjini Beirut kwa miaka sita sasa, ni baada ya kupakuliwa kutoka kwenye meli iliyokamatwa mwaka 2013.

Mzigo huo wa Amonium Nitrate uliwasili kupitia meli iliyokuwa na bendera ya Moldova, ambayo iliingia katika Bandari ya Beirut baada ya kupata tatizo la kiufundi wakati wa safari yake kuelekea Mozambique, kwa mujibu wa tovuti ya Shiparrested.com, ambayo inasimamia masuala ya meli.

Wataalamu katika Chuo Kikuu cha Sheffield, Uingereza wanakadiria kwamba, mlipuko huo ulikuwa na kiwango cha 1/10 cha nguvu za bomu la nyuklia lililoangushwa katika Mji wa Japan wa Hiroshima wakati wa Vita vya Pili vya Dunia na limetajwa kuwa mlipuko mkubwa wa bomu lisilo la nyuklia katika historia.

Meli hiyo ilikaguliwa na kupigwa marufuku kuondoka kwenye bandari hiyo, baadaye iliachwa na wamiliki wake kutokana na tatizo la kisheria. Mzigo wa sumu hiyo ulihifadhiwa katika ghala moja la bandari kwasababu za kiusalama.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!