November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Magufuli atamani Ndugai awe spika tena

Spread the love

JOB Ndugai, Spika wa Bunge la Tanzania, ameanza kupigiwa kampeni za kuongoza Bunge hilo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya uchaguzi mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Dk. John Pombe Magufuli ambaye ni mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema, atashangaa kama Ndugai hatachaguliwa kuongoza bunge hilo.

Dk. Magufuli ametoa kauli hiyo leo tarehe 6 Agosti 2020, wakati akizungumza na wanachama wa CCM baada ya kuchukua fomu ya kugom bea Urais wa Tanzania katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Mbele ya wanachama na viongozi wengine wa chama hicho amesema, atashangaa endapo Bunge linalokuja hatochaguliwa tena kuwa spika wa bunge hilo.

Amesema, Spika Ndugai alisimama imara katika kulinda rasilimali za madini baada ya Bunge lake la 11 kutunga sheria za kulinda rasilimali za madini sambamba na kuunda tume ya kuchunguza upotevu wa madini madini.

“…na ndio maana namshukuru Spika na nitaashangaa sana Bunge linalokuja waache kukuchagua kuwa spika.

Watasema nakufanyia kampeni lakini lazima nikufanyie kampeni, aliunda tume ya kuchunguza madini na kutunga sheria nzuri nchi,” amesema Rais Magufuli.

Mwana 2017, Ndugai aliongoza Bunge hilo kuunda Tume ya Uchunguzi wa shughuli za uchimbaji madini pamoja na biashara ya madini.

Kamati hiyo iliyokuwa na wjaumbe tisa, ilifanya tathimini ya mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa madini ya almasi nchini, kisha kuandaa mapendekezo kwa ajili ya kuishauri Serikali kuhusiana na uendeshaji bora wa biashara ya madini nchini.

Tayari Ndugai amepita katika kura za maoni kugombea Ubunge Jimbo la Kongwa mkoani Dodoma, katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

error: Content is protected !!