Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sasa hivi wathubutu waone – Zitto
Habari za Siasa

Sasa hivi wathubutu waone – Zitto

Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo akizungumza na wananchi wa Kigoma
Spread the love

WIZI wa kura unaolalamikiwa wakati wa uchaguzi mkuu, sasa hautatokea kwa namna Chama cha ACT-Wazalendo kilivyojipanga Bara na Visiwani. Anaripoti Faki Sosi, Kasulu Kigoma … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa na Zitto Kabwe, kiongozi wa chama hicho jana tarehe 8 Julai 2020, wakati akiwa Kasulu kwenye ziara yake ya mikoa ya Magharibi mwa Tanzania.

“Sasa hivi hakutakuwa na bao la mkono, wathubutu kuiba waone. Si wamezoea, sasa kwenye uchaguzi huu waibe,” amesema Zitto.

Kiongozi huyo anayemaliza muda wake wa ubunge katika Jimbo la Kigoma Mjini, amesema ACT-Wazalendo kimejipanga kukabiliana na ‘ujangili’ huo kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Akizungumza na wanachama wa chama hicho, amesema viongozi wa chama hicho wamejifunza kutokana na kile kilichotokea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka jana.

Amesema, chama hicho kimejipanga kuanzi ngazi ya chini hadi taifa kuingia kushiriki uchaguzi na kushinda kwa kishindo na kwamba, chama hicho hakitaibiwa kura zake.

Akizungumzia Tume Huru, Zitto amesema, chama hicho hajijapuuza umuhimu wa tume hiyo na kwamba, kitakwenda kwenye uchaguzi huku kikitafuta Tume Huru.

“Kuna watu wanaenda kujiunga na vyama vyengine kwa sababu CCM imewahidi kuwapa viti, mbona hawakuwapa kwenye serikali za mitaa? Kama hawakupa kijiji, kata? watawapa jimbo?” amehoji Zitto.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!