October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Maalim Seif, majimbo 34 tunachukua Z’bar’

Maalim Seif Sharrif Hamad, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo

Spread the love

MAALIM Seif Sharif Hamad atashinda urais wa Zanzibar na tuna uhakika wa kushinda majimbo 34 ya uchaguzi visiwani humo. Anaripoti Faki Sosi, Kigoma … (endelea).

Hiyo ni kauli ya Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo aliyoitoa tarehe 8 Julai 2020, mbele ya wanachama wa chama hicho Kigoma.

Zitto ameanza ziara yake kwenye Mikoa ya Magharibi, akianzia Kasulu ambapo amefanya vikao vya ndani na kukutana na viongizi wa ngazi mbalimbali pia wanachama wa chama hicho.

“Kule Zanzibar tunashinda majimbo 34, mapema asubuhi Maalim Seif rais Zanzibar, wamezoea kuiba, sasa Maalim Seif yupo chama cha ACT-Wazalendo, waibe waone.

“Tumeimarisha nguvu, uimara ujasiri wa Maalim Seif Hamad unakutana na nguvu ya kijana wenu Zitto kabwe,” Zitto amewaambia wanachama wa chama hicho Kigoma.

Maalim Seif mara kadhaa amenukuliwa akisema, safari hii hana uwezo wa kuwazuia Wazanzibari kupigania haki yao endapo ataporwa ushindi.

error: Content is protected !!