Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Diwani Chadema kugombea ubunge NCCR-Mageuzi
Habari za Siasa

Diwani Chadema kugombea ubunge NCCR-Mageuzi

Mustafa Muro, diwani wa Kinondoni (Chadema)
Spread the love

MUSTAFA Muro, aliyekuwa Diwani wa Kinondoni, jijini Dar es Salaam kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ameomba ridhaa ya kugombea ubunge katika Jimbo la Kinondoni kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Muro ambaye anamaliza muda wake wa udiwani, ametangaza nia hiyo leo Jumatano tarehe 24 Juni 2020, wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam.

Pia amesema, Martha Chilomba, aliyekuwa mwanachama wa Chadema, ametia nia ya kugombea Jimbo la Kawe, jimbo hilo limeongozwa na Halima Mdee (Chadema) kwa miaka 10 (2010-2020).

“Mimi Mustapha Muro, nimetia nia kugombea Kinondoni, bahati mbaya mwenzangu wa Kawe, Martha Chilomba, amepata msiba na ameenda Tabora, pamoja na sisi hapa tunao watia nia wa udiwani,” amesema Murro.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!