Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Tangulizi Uchaguzi 2020: Vita ya ACT-Wazalendo, CUF yaanza upya
Tangulizi

Uchaguzi 2020: Vita ya ACT-Wazalendo, CUF yaanza upya

Spread the love

VITA baina ya Chama cha Wananchi (CUF) na Chama cha ACT-Wazalendo imeanza upya. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Vita hiyo imeanza upya baada ya wabunge 21 na madiwani tisa wa CUF,waliomaliza muda wao, wakiongozwa na Ally Salehe, Mbunge wa Malindi Visiwani Zanzibar, kumejiunga na ACT-Wazalendo.

Wabunge hao wastaafu wamepokelewa leo Jumamosi tarehe 20 Juni 2020 jijini Dar es Salaam, na viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, akiwemo Maalim Seif Sharrif Hamad, Mwenyekiti wake na Zitto Kabwe, Kiongozi wa chama hicho.

Wimbi la wanachama wa CUF kutimkia ACT-Wazalendo ,limeshika kasi tangu mwezi Machi mwaka 2019, baada ya kuibuka kwa mgogoro wa kiuongozi baina ya Maalim Seif , aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, na Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF.

Maalim Seif aliamua kuongoza wafuasi wake kuhamia ACT-Wazalendo, baada ya kuangukia pua katika kesi waliyoifungua Mahakama Kuu ya Tanzania, kupinga kumtambua Prof. Lipumba kama kiongozi halali wa CUF.

Kitendo hicho cha wanachama wa CUF kuhamia ACT-Wazalendo, kimekosolewa na Abdul Kambaya, aliyekuwa Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma wa CUF.

Kambaya amekosoa hatua hiyo akisema kwamba, ACT-Wazalendo haiwezi kukishinda Chama Tawala cha CCM, kwa kuibomoa CUF.

Kambaya ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF na Mkutano Mkuu wa Taifa wa chama hicho, amesema ACT-Wazalendo inajitekenya na kucheka yenyewe.

“Pale ACT inapodhamiria kupambana na CUF badala ya CCM sio tu kuonyesha namna inavyoenzi itikadi yao ya ujamaa na falsafa ya Unyerere, bali pia ni sawa na kujifungia chumbani kisha unajitekenya na kucheka mwenyewe, ukiulizwa unasema tupo wengi. Huwezi kuishinda CCM kwa kuibomoa CUF,” amesema Kambaya.

Awali, akizungumza kwa niaba ya wabunge hao, Salehe amesema wamejiunga na chama hicho baada ya kuona CUF imepoteza nguvu ya kuhimiri vishindo vya siasa vya sasa.

Salehe amesema wanaanza upya ndani ya ACT-Wazalendo, huku akijigamba kwamba wamejipanga kutetea majimbo yao kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.

Aidha, Salehe amesema walitamani kujiunga na ACT-Wazalendo pamoja na Maalim Seif na wafuasi wake kupitia kampeni ya ‘Shusha Tanga, Pandisha Tanga’, lakini walishindwa kutokana na sababu zilizookuwa nje ya uwezo wao.

“Selemani Bungara (Bwege) anamsemo wake anasema tunaanza upya, moto hauzumiki , tunasonga mbele, toka Machi 18 mwaka jana tulikuwa tunataka tuhajiri lakini kwa sababu mbalimbali viongozi wa chama walitaka tubakie hasa kimkakati walitaka tubaki kule,” amesema Salehe na kuongeza:

“Lakini katika kubaki kule tuliona siku na saa haziendi lakini tulishafika, katika medani ya siasa kwenye utaifa kuna uzalendo lakini kwenye suala la chama kuna uti, tulipoteza utii CUF tangu machi 18, lakini kulikuwa na vitisho ili tumtii viongozi na genge lake.”

Licha ya wabunge hao wa CUF kujiunga na ACT-Wazalendo, madiwani tisa nao wametangaza kujiunga na chama hicho.

Kiongozi wa madiwani hao tisa wa CUF, Jumanne Amir Mbunju, aliyekuwa Diwani wa Kata ya Tandale amesema wameamua kujiunga na ACT-Wazalendo, baada ya kuona kinawafaa kulingana na upepo wa kisiasa uliopo.

“Tumeamua kwa moyo wa dhati baada ya kutazama upepo wa kisiasa ulioko sasa kwenye nchi hii tumeona hakuna chama muafaka kinachoweza kuhimiri vishindo, kinachoweza kupambana na changamoto zote tulizonazo hakuna isipokuwa ACT Wazalendo,” amesema Mbunju na kuongeza:

“Na sababu tumejifunza mengi wakati tuko CUF kwa hali halisi iliyoko sasa, kama utang’ang’ania kwenye chama ambacho unakiona kabisa nguvu ,uwezo na hali halisi haifanani na wakati tulio nao, maana yake unajidhurumu wewe mwenyewe.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

Habari MchanganyikoTangulizi

Walimu 5000 Songwe waililia CWT kuwanyima sare

Spread the loveZaidi ya walimu 5000 ambao ni wanachama wa Chama cha...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

error: Content is protected !!