Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Raia wa Armenia kortini kwa kuisababishia Serikali hasara Mil. 44
Habari Mchanganyiko

Raia wa Armenia kortini kwa kuisababishia Serikali hasara Mil. 44

Spread the love

VARDAN MKHITARYAN (47), raia wa Armenia na mwenzake, wamefikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam kwa kosa kuisababishia hasara Serikali kiasi cha Sh. 44 milioni. Anaripoti Faki Sosi ,Dar es Salaam…(endelea).

Mwenzake ni Rosemary Mwemezi (32), Mtanzania .

Leo Jumatatu tarehe 8 Juni 2020, watuhumiwa hao wamesomewa mashtaka sita na Jacqline Nyantoli mbele ya Hakimu Mkazi Augustina Mbando.

Shtaka la kwanza ni la kula njama, linadaiwa kutendwa na washtakiwa wote wawili kati ya tarehe 1 Oktoba 2019 na tarehe 28 Mei 2020 kwenye maeneo tofauti jijini Dar es Salaam, kwa pamoja walikula njama ya kutenda kosa la udanganyifu kupitia vifaa vya mawasiliano ya kieletroniki.

Kosa la pili, limetendwa na mtuhumiwa wa kwanza la kuingiza vifaa vya mawasiliano ya kieletroniki bila kuwa na kibali cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kosa hilo linadaiwa kutendwa tarehe 1 na 30 Oktoba 2019 jijini Dar es Salaam.

Kosa la tatu ni kusimika vifaa vya mawaliano ya kieletroniki bila kibali cha TCRA .

Inadaiwa mshtakiwa Mkhitaryan kutenda kosa hilo kati ya tarehe 1 na 30 Oktoba 2019 maeneo ya Mbezi Beach Dar es Salaam.

Kosa la nne ni kuendesha vifaa vya kieletroniki bila kibali cha mamlaka linamkabili mshitakiwa Mkhitaryan ambaye ni Meneja wa Kampuni ya Classic Mall iliyopo Mbezi Beach Dar es Salaam, anadaiwa kati ya tarehe 10 Oktoba 2019 na Tarehe 28 Mei 2020 aliendesha vifaa hivyo kwa ajili ya kupokea na kuhamisha mawasiliano  ya kimataifa .

Shtaka la tano, ni la kufanya udanganyifu kwa lengo la kukwepa gharama za kupokea na  kuhamisha mawasiliano ya kimataifa .

Shtaka hilo linawakabili watuhumiwa wote na kutendwa tarehe 10 Oktoba 2019, na tarehe 28 Mei 2020 eneo la Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Shtaka la sita  la kutumia vifaa vya  mawasiliano ya kieletrokini bila kuruhusiwa na TCRA linamkabili Mkhitaryan.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kutenda kosa tarehe 10 Oktoba 2019 na tarehe 28 Mei 2020 eneo la Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Shitaka la mwisho  ni kuisababishia Serikali na mamlaka hasara ya kiasi cha Sh. 44, 552, 175.

Kosa hilo linamkabili Mkhitaryan  na anadaiwa kulitenda tarehe 10 Oktoba 2019, na tarehe 28 Mei 2020 eneo la Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwa sababu kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.

Hakimu Mbando ameahirisha kesi hiyo mpaka 10, Juni 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!