Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya CCBRT wajitosa vita ya corona
Afya

CCBRT wajitosa vita ya corona

Spread the love

MKURUGENZI Mtendaji Mkuu wa hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi amekabidhi vifaa maalumu vya kujikinga na virusi vya Corona usoni (Face Shields) vipatavyo 150 kwa hospitali na vituo vya afya 22 katika Manispaa za mkoa wa Dar es Salaam. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Akikabidhi visa hivyo leo tare he 27 Mei, 2020, kwa wawakilishi wa hospitali hizo kutoka Manispaa tano za mkoa wa Dar es Salaam, Brenda amesema lengo ni kuunga mkono juhudi za Serikali na wadau wengine hapa nchini katika kuwakinga wahudumu wa afya na janga la Corona. 

“Tumekusudia vifaa hivi vitumike katika vitengo vya afya ya uzazi katika hospitali hizo ili kuwakinga wahudumu wa afya ambao kila siku wamekuwa mstari wa mbele kuokoa maisha ya mama na mtoto,” amesema.

Amesema kuwa vifaa hivyo vitasaidia kuwaweka salama watoa huduma salama wakati wakiwahudumia wagonjwa.

Kwa takribani kipindi cha miaka 10, CCBRT kwa kushirikiana na Timu ya Afya ya Mkoa wa Dar es Salaam (RHMT) na Timu za Afya za Manispaa (CHMTs), wamekuwa wakiendesha mradi wa kujenga uwezo wa watumishi wa afya eneo la afya ya uzazi katika hospitali, vituo vya afya na zahanati 22 katika Manispaa zote tano za Mkoa wa Dar es Salaam.

wa sasa mradi huu pia unafanya kazi na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Mloganzila hasa kwenye upande wa rufaa za wagonjwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

error: Content is protected !!