Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Madaktari Tanzania watoa tathimini ya ugonjwa wa corona
Afya

Madaktari Tanzania watoa tathimini ya ugonjwa wa corona

Rais wa MAT, Dk. Elisha Osati
Spread the love

CHAMA cha Madaktari Tanzania (MAT), kimewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kubwa ya ugonjwa wa COVID-19 hasa kipindi hiki ambacho wanafunzi wa vyuo na kidato cha sita wanarejea masomoni kuanzia tarehe 1 Juni, 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea)

Pia, MAT imewataka wagonjwa walioko majumbani wenye matatizo ya COVID-19 au magonjwa mengine kwenda hospitalini wahudumiwe, kwani ugonjwa wa COVID-19 umepungua kwa kiasi kikubwa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano tarehe 27 Mei, 2020 jijini Dar es Salaam, Rais wa MAT, Dk. Elisha Osati amesema, licha ya wagonjwa kupungua lakini ugonjwa bado upo na sisi, “madaktari tuko tayari kuwahudumia hivyo, wananchi waje tuwahudumie.”

“Ugonjwa bado upo na tuendelee kuchukua tahadhari kubwa, hasa wakati huu ambao wanafunzi wanarudi vyuooni. Tuendelee kunawa mikono na maji tirurika na sabuni au kutumia vitakasa mikono (sanitizers).”

“Tuendelee kupeana umbali wa angalau miguu mitatu kutoka kwa mtu mwingine na kuvaa barakoa kila tunapokuwa kwenye maeneo ya watu wengi na hasa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini,” amesema Dk. Osati

Rais huyo wa MAT ameiomba Serikali na wadau kuendelea kuhakikisha, “upatikanaji wa vifaa kinga na vifaa tiba uendelee kufanyiwa kazi, kwani vifaa hivi ni muhimu kwa ajili ya kutolea huduma hata kama sio huduma za COVID-19.”

“MAT tunawasihi wadau mbalimbali tuendelee kushirikiana na kama Rais alivyosema misaada mbali mbali ya kupambana na COVID-19 ielekezwe kwa wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto,” amesema

Kuhusu ugonjwa wa COVID-19, Dk. Osati amesema, idadi ya wagonjwa wa COVID-19 imepungua kwa kiasi kikubwa katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma.

“Kupungua kwa wagonjwa wanaohitaji huduma kama za hewa ya Oksijeni. Mwezi wanne kwa sampuli tulizokuwa tukizipeleka maabara takriban asilimia 90 ilikuwa na COVID-19 (positive), kwa sasa tukipeleka sampuli zinazorudi positive ni chini ya asilimia 10,” amesema Dk. Osati.

“Idadi ya wagonjwa pia umepungua kwa kiasi kikubwa ndani ya jamii. Kwa kuangalia idadi ya simu zinazopigwa kwa kuuliza au kuomba msaada wa kitaalamu juu ya wagonjwa wenye dalili kama za COVID-19. Kupungua kwa idadi ya vifo vinavyodhaniwa kusababishwa na COVID-19,” amesema

Dk. Osati ametumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli, “kwa kutuongoza Watanzania kupita vizuri katika kipindi hiki kigumu kwa Taifa. Rais ametuongoza vizuri kwa kutoa mwelekeo mzuri sana kwa Taifa, na tunampongeza sana.”

Pia, Dk. Osati wamempongeza, Waziri Mkuu wa Tanzania, Kasim Majaliwa, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na kamti zake zote chini ya waziri wa wizara hiyo, Ummy Mwalimu  kwa namna wanavyoongoza nchi kupambana na ugonjwa huu wa C0VID-19.

“Tunawapongeza sana madaktari na watumishi wote wa sekta ya afya kwa kuwa askari wa mbele kupambana na COVID-19. Tunatambua kazi wanaendelea kuifanya kwa Taifa letu. Na Mungu awabariki sana,” amesema Dk. Osati

pia, MAT wamewapongeza wadau mbalimbali kwa namna walivyo jitokeza kusaidia juhudi za Serikali katika kupambana na jambo COVID-19.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma

Spread the loveWANAVIJIJI wa Kata ya  Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani...

error: Content is protected !!