Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Michezo Bil 1 za Rais Magufuli zaiweka pabaya TFF
Michezo

Bil 1 za Rais Magufuli zaiweka pabaya TFF

Walace Karia, Rais wa TFF
Spread the love

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), imesema inalichunguza Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kuhusu matumizi mabaya ya fedha, ikiwemo kiasi cha Sh. 1 bilioni kilichotolewa na Rais John Magufuli, mwaka 2019. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 15 Mei 2020, jijini Dar es Salaam na Brigedia John Mbungo, Mkurugenzi wa TAKUKURU, wakati alipoulizwa kuhusu tuhuma za matumizi mabaya ya fedha, zinazolikabili shirikisho hilo.

Brigedia Mbungo ameeleza kuwa, TAKUKURU imeanza kuwahoji watu wanaohisiwa na ubadhirifu wa fedha hizo, pamoja na kukusanya nyaraka za ukusanyaji fedha na matumizi yake.

“Ni kweli Rais Magufuli alitoa fedha kwa ajili ya timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), lakini baada ya rais kuonyesha mfano wa kuchangia, wako wadau wengine waliojitokeza kuchangia fedha. Zile fedha kweli zimetumika vibaya na taasisi inazo taarifa, imechukua hatua za kufanya uchunguzi,” amesema Brigedia Mbungo.

Wakati huo huo, Brigedia Mbungo amewataka wanaohusika na ubadhirifu huo, kurudisha fedha hizo kwa hiari.

“Tunawaita wote wanaohusika au wanahisiwa kuhusika na ugawaji au usimamiaji fedha. Tumeendelea kukusanya nyaraka za ukusanyaji fedha na matumizi yake yaliyofanyika. Huu uchunguzi unaendelea na wa kijinai. Wana hiari ya kurejesha fedha,” amesema Brigedia Mbungo.

Brigedia Mbungo amewataka wadau wa michezo, wenye taarifa juu ya ubadhirifu wa fedha katika sekta hiyo, kuipa taarifa TAKUKURU, ili izifanyie kazi kwa ajili ya kuokoa fedha za umma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

error: Content is protected !!