Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe kuwaongoza wenzake kurejea bungeni leo
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe kuwaongoza wenzake kurejea bungeni leo

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

WABUNGE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), waliotii agizo la chama hicho la kukaa karantini kwa muda wa siku 14, wanatarajia kurejea bungeni leo Ijumaa tarehe 15 Mei, 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mei Mosi, 2020, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, aliagiza wabunge wa chama hicho kutohudhuria shughuli za Bunge,  ili kujikinga au kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosababishwa na virusi vya corona (Covid-19).

Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni alitoa agizo hilo baada ya uongozi wa bunge, kutangaza kwamba, kuna baadhi ya wabunge wameambukizwa ugonjwa wa Covid-19.

Mbowe aliushauri mhimili huo kuwapima wabunge wote na watumishi wake, ili kujua hali ya maambukizi ya ugonjwa huo.

Hata hivyo, Spika wa Bunge, Job Ndugai alipinga ushauri huo akisema shughuli za Bunge zitaendelea kama kawaida huku baadhi ya wabunge wa Chadema nao wakikaidi uamuzi huo wa Chadema na kuendelea kuhudhuria vikao vya Bunge.

Taarifa ya Tumain Makene, Mkuu Idara ya Habari na Mawasiliano imemnukuu John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chadema akisema muda wa kukaa karantini umemalizika na wabunge hao wanarejea kushiriki vikao na shughuli za bunge leo Ijumaa baada ya kuthibitika kwamba hawana mamabukizi ya Covid-19.

 “Wabunge wetu wote waliotekeleza makubaliano na uamuzi wa chama na wabunge, kujitenga kwa siku 14, ambayo yanatokana na maelekezo na ushauri wa wataalamu wa afya, leo watarejea bungeni kuendelea na shughuli za kuwawakilisha wananchi,” amesema Mnyika.

Taarifa ya Chadema kurejea bungeni leo

Mnyika amesema wabunge hao wataendelea kuzingatia tahadhari zote za kujikinga dhidi maambukizi ya Covid-19, wakiwa bungeni.

Jumatano ya tarehe 13 Mei, 2020, Spika Ndugai alitoa orodha ya wabunge 15 wa Chadema akiwataka kutekeleza maagizo yake kabla ya kuruhusiwa kuingia bungeni.

Maagizo hayo, mosi ni; kuwataka kurejea bungeni au kurudisha fedha walizolipwa mara moja.

Pili, kwa kuwa haijulikani wabunge hao walipo, watalazimika kuwasilisha ushahidi kwamba wamepimwa na hawana maambukizi ya virusi vya Covid-19 kabla ya kuruhusiwa kuingia Bungeni.

Wabunge hao na majimbo yao kwenye mabano ni; Freeman Mbowe (Hai), Ester Bulaya (Bunga Mjini), Halima Mdee (Kawe), John Heche (Tarime Vijijini), Joseph Mbilinyi maarufu Sugu (Mbeya Mjini), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini), Pascal Haonga (Mbozi) na Joseph Haule maarufu Profesa J wa Mikumi.

Wengine ni; Rhoda Kunchela, Catherine Rage, Devotha Minja, Joyce Mukya, Aida Joseph Khenan, Upendo Peneza na Grace Kiwelu wote wa viti maalum.

Spika Ndugai aliagiza Kitengo cha usalama cha Bunge kutowaruhusu wabunge hao 15 kutoingia bungeni kuanzia Jumatano tarehe 13 Mei 2020 mpaka watakapotimiza maagizo hayo mawili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!