Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Askofu awatwisha mzigo wa Corona waandishi wa habari
AfyaHabari Mchanganyiko

Askofu awatwisha mzigo wa Corona waandishi wa habari

Spread the love

ASKOFU Evance Chande wa Kanisa la EAGT Dodoma, ameviomba vyombo vya habari na waandishi wa habari kutoa elimu ya maambukizi ya corona kwa wananchi waishio vijijini. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Askofu Chande ametoa kauli hiyo wakati wa Ibada ya kumbukizi ya kufufuka kwa Yesu Kristo iliyofanyika kanisani hapo lililipo Ipagala Jijini hapa.

Alisema kuwa changamoto kubwa iliyopo kwa sasa ni kutokuwepo kwa elimu ya kutosha hasa watu waishio vijijijini.

Akihubiri kanisani hapo alisema iwapo waandishi nao watatumia nafasi yao kwenda vijijini kwa ajili ya kusaidia jamii juu ya kujikinga na maabukizi hayo watakuwa wameisaidia serikali kwa hatua kubwa.

“Hapa mtaona kuwa baada ya Serikali kutangaza kuwepo kwa ugonjwa huo waandishi wa habari na vyombo vya habari vilijitahidi na vinaendelea kujitahidi kutangaza jambo ambalo limesababisha kila mmoja kujua kinachoendelea.

“Vyombo vya habari na waandishi wa habari kwa kutumia weledi wao wanaweza kuwa msaada mkubwa kwa jamii kwa kutoa elimu hata maeneo ambayo hayafikiki,”alisema Askofu Chande.

Katika hatua nyingine amewakemea baadhi ya watu ambao wanafanya mzaa na janga hilo la Corona na kuwataka kuacha mara moja na badala yake wazingatie maelekezo ya Serikali.

Alisema Ugonjwa wa Corona siyo wa mchezo na ni janga la Kidunia hivyo ni muhimu kuhakikisha jamii inazingatia maelekezo ya wataalamu wa Afya.

Akizungumzia kuhusu sikukuu ya kumbukizi ya kufufuka Yesu Kristo alisema siku hiyo isitumiwe kufanya anasa badala yake siku hiyo iwe siku ya kumtafakari Mungu.

Katika hatua nyingine amewaagiza watanzania kwa ujumla wake wakakikishe kwenye majumba yao wanaweka vitakatisha mikono ili wanapotembelewa na wageni wawezi kunawa Kama yalivyo maelekezo ya Serikali.

Naye Askofu wa Kanisa la Pentecostal Holiness Association Mission Tanzania (PHAMT), Jimbo la Kanda ya Kati, Julias Bundala aliiomba serikali kuongeza ulinzi mipakani ili kukabiliana na watu ambao wanaingia nchini na Virusi vya Ugonjwa wa Corona.

Mbali na hilo alisema kuwa serikali iangalie namna bora ya kuwapatia huduma waliowekwa karantini ili wanapokuwa katika ungalizi wa siku 14 wasitoke na badala yake huduma ziwakute hapo hapo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

error: Content is protected !!