Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Mashinji aonja machungu Chadema
Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mashinji aonja machungu Chadema

Spread the love

SIKU sita baada ya Dk. Vicent Mashinji, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), leo ameonja machungu. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Akiwa katika Mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kuhudhuria kesi ya uchochezi Na. 112/2018 inayowakabili yeye na viongozi wa Chadema leo tarehe 24 Frebruari 2020, Dk. Mashindi alijikuta katika wakati mgumu baada ya kutengwa na baadhi ya watu na viongozi wa chama hicho.

Baada ya kufika, Dk. Mashinji alisalimia wanachama na viongozi wa Chadema, lakini alipofika kwa Halima Mdee, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la chama hicho (Bawacha), aligoma kumpa salamu.

Baada ya Mdee akugoma kupokea mkono wa salamu wa Dk. Mashinji, alilazimika kwenda kujitenga pembeni, tofauti na ilivyokua awali alipokuwa Chadema, ambapo walikuwa wanakaa pamoja wakisubiri kuitwa kizimbani kwa ajili ya kusikiliza kesi yao.

Hata alipokuwa ndani ya mahakama, Esther Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini alipoingia ndani ya mhakama ya Kisutu na kusalimia watu aliowakuta, lakini alipofika kwa Dk. Mshinji ambaye naye aliinua mkono ili kugongesha na mkono wa Matiko, alikwepwa.

Baadhi ya wabunge ambao hawakuonesha kumtenga Dk. Mashinji ni pamoja na Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini ambaye alionekana kuzungumza naye a kutoonesha dalili yoyote tofauti.

Dk. Mashinji pamoja na viongozi nane wa Chadema, wanakabiliwa na mashitaka 13 katika kesi hiyo, ikiwemo uchochezi.

Miongoni mwa viongozi wa Chadema wanaokabilia na mashtaka hayo ni, Freeman Mbowe, Mwenyekiti Chadema; John Mnyika, Katibu Mkuu wa chama hicho; Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Chadema Zanzibar na Matiko ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Serengeti.

Hata hivyo, mahakama hiyo imeeleza kwamba inatarajia kutoa hukumu ya kesi hiyo tarehe 10 Machi 2020.

Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka na ule wa utetezi, amesema kuwa anatoa siku tano za kazi kwa mawakili wa pande zote mbili kuwasilisha hoja za majumuisho kwenye shauri.

Hakimu Simba amesema, mahakama ilitoa maelekezo ya kuchapisha nyaraka zote tangu kesi ilipoanza hadi ilipofikia.

“Mpaka kesho mchana (tarehe 25 Februari 2020), nyaraka ziwe zimekamilika zianze kugaiwa kwa pande zote mbili ili waweze kuzipitia kwa ajili ya kuandaa majumuisho yao,” amesema.

Hakimu Simba amesema, mwisho wa kuwasilisha hoja hizo ni tarehe 3 Machi 2020, ambapo upande utakaochelewa kufanya hivyo, atayaondoa majumuisho yao na kwamba sio hitaji la lazima kisheria.

“Kwa mujibu wa sheria pande zote mbili zina haki ya kuomba kufanya majumuisho ya kesi yao ili kusaidia mahakama kufanya uamuzi,” ameeleza Hakimu Simba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!