April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Bashiru amtia kiburi Mwambe

Spread the love

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally amewaaminisha wakazi wa Jimbo la Ndanda, mkoani Mtwara kwamba, hilo litarejea CCM. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mtwara … (endelea).

Amesema, kwa kuwa Cecil Mwambe, aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amerejea CCM ‘hakuna shaka’ jimbo hilo nalo litarejea kwenye chama hicho katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Amemchora Mwambe kama ndio ‘mmiliki’ wa jimbo hilo, akimpa kazi, kwamba wale alioondoka na kujiunga nao Chadema mwaka 2015, awaraejeshe.

Dk. Bashiru ametoa kauli hiyo tarehe 23 Februari 2020, Ndanda wakati wa mapokezi ya Mwambe baada ya kurudi kwenye chama hicho alichokihama mwaka 2015.

Hata hivyo, kiongozi huyo wa CCM aeonesha hofu ya kuibuka kwa makundi, baada ya Mwambe kurejea kwenye chama hicho hususani jimbo la Ndanda.

“…kurudi kwao ndani ya CCM kusiwe chanzo cha makundi ndani ya chama,” amesema Dk. Bashiru na kuongeza “muwasamehe wanachama wote ambao walikihama chama, na hivi sasa wameamua kurejea kwa vile wamekubali makosa yao.”

Baada ya kukabidhi kadi ya uanachama ya Chadema, Mwambe amesema kilichomvutia CCM ni namna chama hicho kinavyotekeleza miradi mikubwa ya maendeleo.

Amedao mbele ya CCM na viongozi wake kwamba, katika miaka mine aliyoishi akiwa mwana Chadema, hakuwa na uhuru wa kutoa mawazo yake, na kwamba ilikuwa kikwazo cha kuwatendea haki wananchi wa Ndanda.

error: Content is protected !!