Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe awaangukia viongozi wa dini
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe awaangukia viongozi wa dini

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amewaomba viongozi wa dini kuliombea taifa, ili liwe salama kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Pwani … (endelea).

Mbowe ametoa wito huo kwenye ibada maalumu ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Mzee Elias Mwingira,  Baba wa Nabii na Mtume wa Kanisa  la Huduma ya Efatha, Josephat Mwingira, leo tarehe 22 Februari 2020, Kibaha mkoani Pwani.

Kiongozi huyo wa Chadema amewaomba viongozi wa dini zote nchini, kuungana kwa pamoja katika kumuomba Mungu, ili uchaguzi huo ufanyike kwa amani.

“Ombi langu maalum kwako Nabii na Mtume Josephat Mwingira, wewe na viongozi wengine kutoka dini zote, mkaungane kuliombea taifa katika mwaka huu wa uchaguzi,” ameomba Mbowe.

Wakati huo huo, Mbowe amewaomba viongozi wa dini kuwaombea viongozi wa vyama siasa ili Mungu awape unyenyekevu.

“Pia mkatuombee sisi  Viongozi wa kisiasa tuache viburi, tuvae unyenyekevu, tukawe na tume huru ya uchaguzi katika uchaguzi ujao, haki ikatamalaki” amesema Mbowe.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!