Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tanzania yapekuwa mikataba ya misaada
Habari za Siasa

Tanzania yapekuwa mikataba ya misaada

Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Profesa Adelardus Kilangi
Spread the love

 SERIKALI ya Tanzania kupitia Ofisi ya Mwansheria Mkuu (AG), inapitia upya mikataba ya misaada na mikopo takribani 70, ili kuangalia masharti yake kama yana tija kwa taifa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Adeladius Kilangi wakati akizungumza katika maadhimisho ya Wiki ya Sheria yaliyofanyika leo tarehe 6 Februari jijini Dar es Salaam.

AG Kilangi ameeleza kuwa, ofisi yake inarejea mikataba hiyo ili kuangalia kama masharti yake  yana tija kwa taifa, ikiwemo sharti la kusamehe mambo mbalimbali.

“Ofisi ya AG inafanya rejea pia,  kwenye baadhi ya mikataba ya misaada na mikopo ipatayo 70.  Ili kuangalia tija ya baadhi ya masharti ikiwiemo sharti la ksuamehe mambo mbalimbali,” amesema AG Kilangi.

Wakati huo huo, AG Kilangi amesema ofisi yake imepitia upya mikataba 13 ya uwekezaji, utafutaji na uzalishaji mafuta na gesi., na kwamba imekwishawasilishwa kwa Mwanasheria Mkuu.

Pia, Ofisi ya AG imepitia mikataba 182 ya uwekezaji yenye utata, kati ya wawekezaji na mashirika ya umma.

“Hivi karibuni ofisi ya mwanasheria mkuu itaanza kurejea mikataba yote ya uwekezaji, kati ya nchi mbili na uwekezaji katika ya nchi mbalimbali ambayo inaihusu Tanzania, “ amesema AG Kilangi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!