Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waombewe wapate laana – Rais Magufuli
Habari za Siasa

Waombewe wapate laana – Rais Magufuli

Rais John Magufuli
Spread the love

UKOSEFU wa maadili, tabia ya kuchelewesha kesi kwa makusudi na kuendekeza rushwa katika Mahakama za Tanzania, kunamkwaza Rais John Magufuli. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea). 

Akizungumza kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria, jijini Dar es Salaam leo tarehe 6 Februari 2020, Rais Magufuli ameshauri viongozi wa dini wawaombee wanaofanya vitendo hivyo wapate laana.

“Niwaombe viongozi wa dini, kaliombeeni sana suala hili ili wale wanaochelewesha kwa makusudi, wakapate laana ili Mungu akaanze kuwaadhibu wao, kabla ya wale waliowaweka mahabusu,” amesema Rais Magufuli.

Amesema, kuna tatizo la kukosekana kwa maadili ikiwemo kubambikia watu kesi, jambo ambali linavuruga taswira ya mahakama, na kwamba kila mmoja anawajibika kukosoa dosari hizo.

“Kuna matatizo ya kukosekana kwa maadili, ikiwemo kuendeleza vitendo vya rusha kwa kubambikiza kesi kama nilivyosema.

 Tuna wajibu wa kukosoa hizo dosari sisi wote kwa pamoja na kumtanguliza Mungu ili watu wasikosee,” amesema.

Ameeleza changamoto nyingize inayoikumba Mahakama za Tanzania, nikuendelea kukithiri kwa migogoro ya ardhi, na kwamba waathirika wakubwa wamekuwa wanawake hususani wajane.

Amesema, amekuwa akifanya ziara maeneo mbalimbali ya nchi, miongoni mwa mambo makubwa anayokumbana nayo ni migogoro ya ardhi.

Hivyo, ameyataka Mabaraza ya Ardhi kushirikiana na wadau wengine kuhakikisha haki inatendeka, huku akishuri kuundwa kwa timu maalum ya kushughulikia matatizo hayo.

Anasema, hana hakika kama Mabaraza ya Ardhi yanafanya kazi vizuri, na kwamba serikali inawezekana ilifanya makosa kuyaacha yakiwa huru.

“Lakini pale lawama zinapotokea, inanyooshewa kidole mahakama,” amesema huku akisema mabaraza hayo badala ya kuwa chini ya Wizara ya Ardhi, yawe chini ya mahakama ili yashughulikiwe vizuri.

“Kwenye Mabaraza ya Ardhi kuna kelele nyingi, wale watu kule wanapindua wanavyotaka, mimi nimekaa Wizara ya Ardhi, nafahamu,” amesema Rais Magufuli.

Pia kiongozi huyo wa nchi, ameipongeza mahakama kwa kufanya kazi nzuri na yenye mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuimarisha mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

“Naipongeza sekta ya sheria na mahakama nchini kwa kupata mafanikio makubwa, ikiwemo kupungua kwa muda wa usikilizwaji wa kesi, kuimarisha matumizi ya TEHAMA pamoja na kuanzisha mahakama zinazotembea,amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!