October 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbowe: Majibu yenu yataleta majuto

Spread the love

FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, amemweleza Kasim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania kuwa majibu mepesi yanayotolewa kuhusu Tume Huru ya Uchaguzi, yataleta majuto. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Kambi Rasmi Bungeni, ametoa kauli hiyo wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, leo tarehe 6 Februari 2020.

Kiongozi huyo amesema hivyo baada ya Waziri Mkuu, Majaliwa kulieleza Bunge, kwamba Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2019, ulikuwa huru na haki jambo lililofanya Taifa kuwa na shwari.

Kufuatia majibu hayo, Mbowe amesema majibu yanayotolekwa na serikali juu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kwamba iko huru kwa mujibu wa Katiba na Sheria, itakuja kuleta majuto kwa taifa.

“Unajua vizuri tume sio huru na watendaji sio huru. Matendo yamejitokeza wazi yanaonekana, haya ni majibu mepesi ambayo kuna siku mtakuja kujuta kwenye nchi hii kwa majibu haya mepesi.” amesema Mbowe.

Mbowe ameishauri serikali kuanzisha mchakato wa upatikanaji wa Tume Huru ya Uchaguzi, pamoja na kuviacha huru vyama vya siasa vya upinzani kufanya shughuli zake za uenezi wa chama.

“Unajua vizuri sana serikali, Watanzania, wanajua vizuri sana kwamba vyama vya upinzani vimezuiwa kwa miaka minne kufanya kazi zake za uenezi. Unapotupa maelezo ndani ya bunge kuhalalisha kilichofanyika (Uchaguzi Serikali za Mitaa 2019) na kusema ni utaratibu mliojiwekea kwa sheria ipi?” amehoji Mbowe na kuongeza:

“Waziri Mkuu hamuoni ni muda muafaka serikali ikaona umuhimu wa wadau wanaohusika na masuala ya uchaguzi, kukaa kutafuta njia nzuri ya kwenda kwenye uchaguzi kuliko kwenda kibabe.”

Akijibu majibu ya Mbowe, Waziri Majaliwa amekanusha kwamba serikali inaendeshwa kibabe, huku akisisitiza kuwa, NEC iko huru kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi, na wala haiingiliwa na rais wala mamlaka yoyote ile.

Aidha, Waziri Majaliwa amemshauri Mbowe kama utendaji wa NEC una dosari, apeleke changamoto hizo kwenye mamlaka husika kwa ajili ya kufanyiwa kazi.

“Tume kutokuwa huru ni mtizamo wa mtu, lakini kikatiba na utendaji wake iko huru na pale ambako kunaonekana kuna shida ielezwe hapa kuna shida lakini hatujawahi kuona rais anaingilia wala chama cha siasa. Ile tume iko huru na inafanya kazi yake kama ilivyotakiwa kwa mujibu wa katiba, ukiwa na jambo lolote unaweza kusema ili tuone wapi tusaidie kusudi jambo hilo liende sawasawa, “amehimiza Waziri Majaliwa.

Akijibu kuhusu vyama vya upinzani kuzuiwa kufanya shughuli za siasa, Waziri Majaliwa amesema hakuna mbunge anayezuiwa kufanya mikutamno katika jimbo lake, na kushauri wabunge wanaokutana na changamto hizo, kuzifikisha katika mamlaka husika kwa ajili ya utatuzi.

“Nikanushe kwamba serikali inaongozwa kibabae, haiongozwi kibabe. Mbowe ni kiongozi tunazungumza tunabadilishana mawazo lakini sote tunapobalishana mawazo tunalenga kulifanya taifa liwe na usalama,” ameeleza Waziri Majaliwa na kuongeza:

“Hakuna mbunge aliyezuiliwa kufanya siasa na watu wake, inawezekana kuna tatizo sehemu fulani tuambizane kuna shida kama zipo wkenye ngazi ndogo ni suala la kutatua, pale kwenye shida namna hiyo tuendelee kuwasiliana.”

error: Content is protected !!