Monday , 6 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Familia ya Kabendera hali mbaya, kampeni ya kuichangia yaanzishwa
Habari Mchanganyiko

Familia ya Kabendera hali mbaya, kampeni ya kuichangia yaanzishwa

Spread the love

KUFUATIA hali mbaya ya kiuchumi inayopitia Familia ya Mwanahabari Erick Kabendera, aliyeko mahabusu kwa zaidi ya miezi mitano katika Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam, kampeni ya kuiwezesha familia hiyo yaanzishwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kampeni hiyo ya mtandaoni iliyopewa jina la ‘Saidia Familia ya Erick Kabendera’ ilianzishwa jana tarehe 14 Januari 2020 katika mtandao wa ‘GoFundMe’, na inaratibiwa na Selma Steenhusein akishirikiana na Imma Mbuguni, pamoja na dada wa mwanahabari huyo, Prisca Kabendera.

Lengo la kampeni hiyo ni kuchangisha fedha kupitia mfuko unaopatikana katika mtandao wa Gofundme, ambapo fedha hizo zitatumika katika kusaidia familia ya Kabendera.

“Mfuko huu umeanzishwa kuisadia familia ya Kabendera katika kipindi hiki kigumu inachopitia,” inaeleza taarifa iliyochapishwa katika mtandao wa Gofundme, kuhusu kampeni ya kuichangia familia ya Kabendera.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, fedha zitakazopatikana zitapelekwa moja kwa moja kwa familia husika, ili iweze kujikimu katika kugharamia huduma za matibabu pamoja na za kisheria dhidi ya Kabendera.

“Fedha hizo zitaisadia familia ya Kabendera inayokabiliwa na gharama za huduma za kisheria, matibabu ya Erick, pamoja na matumizi ya kila siku ya familia hiyo, ikiwemo chakula, maji, ada za watoto, madeni pamoja na gharama za usafiri wa kwenda kumuona na kumpelekea chakula Erick mahabusu,” inaeleza taarifa hiyo.

Kabendera alikamatwa tarehe 29 Julai mwaka jana, ambapo anatuhumiwa kukwepa kodi, uhujumu uchumi, pamoja na kutakatisha fedha Sh. 173.2 milioni, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tanzania  yasisitiza kuwa Kituo Kikuu cha Uchimbaji Madini Afrika

Spread the loveTanzania imeendelea kusisitiza adhma yake ya kuwa kituo kikuu cha...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

error: Content is protected !!