Sunday , 5 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto, Mbowe, Kabendera watajwa ripoti ya Amnesty
Habari za SiasaTangulizi

Zitto, Mbowe, Kabendera watajwa ripoti ya Amnesty

Spread the love

SERIKALI ya Rais John Magufuli, imeshauriwa kubadili mwelekeo wake, ikiwa ina dhamira ya kweli katika kuimarisha uhuru na demokrasia nchini. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Pia, serikali imetakiwa kuimarisha ulinzi wa haki za binadamu, sambamba na kuacha kutumia sheria kandamizi dhidi ya haki za binadamu.

Ripoti ya Shirika la Kimataifa la Kutetea haki za Binadamu la Amnesty, iliyotolewa leo tarehe 28 Oktoba 2019, imeeleza udhaifu katika kusimamia demokrasia na uhuru wa kujieleza nchini.

“Amnesty inaitaka Serikali ya Tanzania kuacha kutumia sheria kandamizi, kukiuka haki za binadamu. Haki ya uhuru wa kujieleza, kupokea na kutoa taarifa, haki ya kukusanyika na mikutano ya amani,” imeeleza ripoti hiyo.

Shirika hilo Limeitaka serikali kuwaacha huru bila masharti, washtakiwa wa kisiasa, wanaharakati na wanahabari.

Waliotajwa kwenye ripoti hiyo ni Zitto Kabwe, Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo; Freema Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema); Dk Vincent Mashinji, Katibu Mkuu Chadema; Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Chadema Bara.

Wengine ni Peter Msigwa, Iringa Mjini; Esther Matiko, Tarime Mjini; Halima Mdee, Kawe; John Heche, Tarime Vijijini; Ester Bulaya, Bunda Mjini pamoja na wanahabari Erick Kabendera na Maxence Mero.

Shirika hilo limemshauri Rais Magufuli kuhakikisha mamlaka zilizoko chini yake, zinawapa uhuru watetezi wa haki za binadamu, wanasiasa, wanahabari na makundi mengine, kutumia haki zao za msingi, ikiwemo uhuru wa kujieleza, uhuru wa kukusanyika pasina hofu.

“Rais ahakikishe mamlaka zinaruhusu kila mmoja, ikiwemo wanasiasa wa upinzani, wanahabari, watafiti, watetezi wa haki za binadamu, kutumia haki zao, ikwiemo haki ya uhuru wa kujieleza, uhuru wa kukusanyika.

“Kuhakikisha mamlaka zinaondoa zuio la mikutano ya vyama vya siasa, na kuwapata uhuru kila mmoja kufurahia haki yake, kukusanyika na kufanya mikutano ya amani.”

Amnesty imeitaka Serikali ya Tanzania kuimarisha haki za binadamu kabla, wakati na baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa wa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa 2020.

“Tunatoa wito, kurekebisha Sheria ya Vyama vya Siasa, Sheria ya Takwimu, Sheria ya Uhalifu wa Mtandao, Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari na Mashirika yasiyo ya kiserikali NGO,” imependekeza ripoti hiyo.

Wakati huo huo, Amnesty imetoa wito kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuondoa sheria zinazokinzana na misingi ya haki za binadamu.

“Mapendekezo kwa Bunge, kuondoa sheria zote zinazokandamiza haki binadamu kabla, wakati na baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2019 na uchaguzi mkuu wa 2020.

“Wito kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhakikisha vyombo vya habari vinafanya kazi zake kwa uhuru na kufurahia uhuru wa kujieleza na kufanya kazi zao pasipo hofu,” imependekeza Amnesty.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

error: Content is protected !!