Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 24 – Serikali
Habari za SiasaTangulizi

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 24 – Serikali

Spread the love

KITENDAWILI kuhusu tarehe rasmi ya kufanyika kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini, sasa kimeteguliwa. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Seleman Jafo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), ametangaza kuwa tarehe 24 Novemba 2019 ndio siku ya kufanya uchaguzi huo leo tarehe 23 Agosti 2019 jijini Dodoma.

 “Kwa mujibu wa kanuni za uchgauzi wa serikali za mitaa mwaka 2019 ibara ya 4 ibara ndogo ya 1 na 3, waziri mwenye dhamana ya tawala za mitaa na serikali za mitaa anawatangazia umma na vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu kuwa, uchaguzi ni tarehe 24 Novemba 2019,” amesema Jaffo.

Akielezea sehemu ya ratiba ya zoezi hilo, Jaffo amesema upigaji kura utaanza majira ya saa 2.00 asubuhi na kumalizika saa 10 Alasiri.

Amesema, wasimamizi wa uchaguzi watatoa maelekezo ya uchaguzi huo siku 62 kabla ya siku ya uchaguzi, wakati watumishi watakaosimamia zoezi la uandikishaji na uandaaji orodha ya wapiga kura  watateuliwa siku 52 kabla ya uchaguzi.

Pia, amesema uandikishaji na uandaaji orodha ya wapiga kura utaanza siku 47 kabla ya uchaguzi siku ya uchaguzi huo ambapo zoezi hilo litafanyika ndani ya siku saba. Fomu za uteuzi zitachukuliwa siku 26 kabla ya siku ya uchaguzi na wahusika watarejesha fomu hizo ndani ya siku saba tangu siku ya kwanza ya kuchukua.

“Ukomo wa madaraka katika nafasi zote zilizogombewa mwaka 2014, viongozi hao watakoma kushika nafasi ya uongozi siku saba kabal ya siku ya wagombea kuchukua fomu ya uteuzi,” amesema Jaffo.

Jaffo amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi katika zoezi la uandikishaji na upigaji kura kwa ajili ya kuchagua viongozi bora.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

error: Content is protected !!