Tuesday , 16 April 2024
Home Habari Mchanganyiko  ATCL yatangaza mabadiliko ya ratiba za ndege
Habari Mchanganyiko

 ATCL yatangaza mabadiliko ya ratiba za ndege

ATCL Dreamliner
Spread the love

SHIRIKA la Ndege la Tanzania (ATCL) leo tarehe 24 Agosti 2019 limetangaza mabadiliko ya ratiba zake za safari za ndege. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

ATCL imetangaza mabadiliko hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, huku likieleza kwamba hatua hiyo inatokana na sababbu zilizo nje ya uwezo wake.

Hata hivyo, shirika hilo halijaweka wazi mabadiliko ya ratiba zake, na kuishia kuwaomba radhi wateja wake kwa usumbufu utakaojitokeza kwenye mipango yao ya safari.

“Wapendwa wateja wetu, kutokana na sababu zilizopo nje ya uwezo wetu, Air Tanzania inasikitika kuwa taarifu kuwa kutakuwa na mbadiliko ya ratiba za ndege. Tuna waomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza kwenye ratiba/mipango ya safari zenu,” inaeleza taarifa ya ATCL.

Taarifa hiyo ya ATCL imekuja siku moja baada ya Mhandisi Isack Kamwelwe, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi kueleza kwamba ndege ya shirika hilo imezuiwa nchini Afrika Kusini kwa amri ya Mahakama Kuu ya Gauteng iliyoko Johannesburg nchini humo.

“Kwa mujibu wa taarifa ambazo serikali imepokea kutoka kwa balozi wetu nchini Afrika Kusini, ndege imezuiwa kwa amri ya mahakama. Serikali kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu inafuatilia suala hilo ili ndege hiyo iachiwe mara moja na kuendelea na safari zake kama kawaida,” amesema Mhandisi Kamwelwe.

https://twitter.com/AirTanzania/status/1165101305435742208

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Sekta binafsi yasifu utekelezaji wa Mkumbi

Spread the loveSERIKAL imepongezwa kwa utekelezaji wa mapendekezo ya sekta binafsi kupitia...

Habari Mchanganyiko

Kamati ya bunge yapigia chapuo kilimo ikolojia

Spread the loveSERIKALI kupitia Wizara ya Kilimo imeshauriwa kushirikiana na wadau wa...

Habari Mchanganyiko

Serikali yapata hasara 113 milioni hospitali kuwapa misamaha wagonjwa wasiostahili

Spread the loveSERIKALI imepata hasara ya kiasi cha Sh. 111.76 milioni, baada...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

error: Content is protected !!