SERIKALI kupitia Wizara ya Malisili na Utalii imeshauriwa kuhakikisha inaendeleza na kutangaza vivutio ambavyo vinaonekana kusaulika kama vile michoro ya mapangoni iliyopo Usandaweni Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma. Anaripoti Danson Kaijage, Chemba … (endelea).
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Gawa Best Vision, Aloyce Malogo, alipokuwa akizungumza na wananchi pamoja na vyombo vya habari katika tamasha la kukuza na kuenzi utalii wa michoro ya mapangoni iliyopo usandaweni eneo la Sanzawa katika wilaya ya Chemba.
Alisekuwa Tanzania inayo vivutio vingi na vya kutosha lakini kwa sehemu moja au nyingine serikali kupitia Wizara husika imekuwa ikishindwa kuviendelea na kuviacha vikasaulika.
Alisema yeye kama Mkurugenzi wa Gawa Best Vision na Mratibu wa Tamasha la kukuza na kuhamasisha kuenzi utalii wa ndani kupitia michoro ya mapangoni iliyopo Usandaweni kata ya kwa Mtoro, anaiomba serikali kuhakikisha inakuza utalii wa ndani kwa kuweka mazingira bora ya kuifanya michoro hiyo kuwa sehemu ya utalii.
Gawa alisema kuwa ili nchi iweze kuwa na uchumi mkubwa kupitia katika Wizara ya Maliasili na Utalii ni vyema kuhakikisha vyanzo vyote vya utalii vinaboreshwa na kutangazwa kwa lengo la kuwavutia watalii ambao wanaweza kuvutiwa na kufika kuangalia jambo ambalo linaweza kuongeza kipato.
Alisema kuwa yeye akiwa mzaliwa wa eneo la Usandaweni ambako kuna michoro na amekuwa akifuatilia kwa karibu sana huku rasilimali nyingi za kiutalii hazitumiki na kuanzisha uhamasishaji wa wadau mbalimbali ili kuhakikisha wanajitokeza kwa lengola kutaka kukuza utalii.
Hata hivyo alisema kuwa katika maeneo ya Usandawe kuna michoro zaidi ya 28 ya aina mbalimbali kwa ambayo kama ikitangazwa vizuri inaweza kusababisha uwepo wa watalii na kuongeza kipato.
Kwa upande wake wananchi wa maeneo ya Usandawe ambako kuna michoro hiyo, Amina Kisua amesema kuwa kwa upande wa utamaduni umekuwa ukipewa thamani kubwa na wazungu lakini wazawa ambao ni watanzania wanakuwa hawaoni thanani yake.
Kutokana na hali hiyo, Amina aliitaka serikali kuona uwezekano wa kuboresha maeneo yote yenye kuwa na mambo ya kale ili yaingizwe kwenye idadi ya vivutio ambavyo vitaidia kuongeza pato la Taifa.
Naye Ayubu Seleli, mkazi wa kijiji cha kwa Mtoro, alisema kuwa inasikitisha kuona kuwa vijana wengi kujikita zaidi katika masuala ya utandawazi au mitindo kutoka mataifa mengine na kusahau utamaduni wa nchini mwao.
Alisema kuwa inasikitisha kuona kuwa vijana wengi wameshindwa kutangaza vivutio vingi ambavyo vipo Usandaweni na kusababisha kukosekana kuongezeka kwa pato pa taifa kwani kama vivutio hivyo vingetangazwa vingeongeza pato.
Kutokana na hali hiyo Seleli ametoa wito kwa vijana wanaotokea Usandaweni kuhakikisha wanatangaza utalii wa ndani hususani katika eneo la Usandaweni ili kufanya sehemu hizo ziendelee kuneemeka na kujiingizia kipato.
Leave a comment