Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waziri amkingia kifua ‘boss’ wake
Habari za Siasa

Waziri amkingia kifua ‘boss’ wake

Luhaga Mpina, Waziri wa Mifugo na Uvuvi
Spread the love

LUHAGA Mpinda, Waziri wa Mifugo na Uvuvi amelalamikia watu anaodai, wanataka kumng’oa Rais John Magufuli asigombee kwenye uchaguzi mkuu 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Malwilo, Tindabuligi jimboni kwake Kisesa, Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu, Mpina amesema watu wanaomsakama Rasi Magufuli ambaye ni mwenyekiti wa chama chao, ni wale waliokuwa na nyadhifa za juu serikalini na kwenye chama hicho.

Mpina amesema, pamoja na watu hao kupanga mikakati ya kumkwamisha ‘boss’ wake, mikakati hiyo haitafanikiwa.

Akizungumzia mikakati hiyo Mpina amesema, viongozi hao waliwahi kupewa nafasi za juu ndani ya CCM na Serikali, lakini Watanzania walishuhudia usimamizi dhaifu wa shughuli za chama na kusababisha makundi makubwa ndani ya chama hicho.

“Walanguzi na wala rushwa waliokuwa wanaiba fedha za taifa hili wamedhibitiwa, mishahara hewa ililipwa miaka nenda rudi viongozi wakawa wanaiba mishahara hewa kana kwamba hakuna mtu aliyetakiwa kuchukua hatua… leo Mheshimiwa John Magufuli amekuja, mishahara hewa yote imekuwa historia,” amesema Mpina na kuongeza:

“Uvuvi haramu ulikuwa kila kona, samaki walikuwa hakuna Taifa lenye maziwa makubwa kuliko nchi yoyote Afrika na Dunia, Taifa lenye bahari samaki tunanunua za kutoka nje. Mheshimiwa Magufuli akasema uvuvi haramu hapana, Mpina nenda pale kakomeshe uvuvi haramu, uvuvi haramu umekoma nchi hii,” amesema.

Amesema, kwa sasa Tanzania inashuhudiwa mageuzi makubwa aliyoyafanya Rais Magufuli katika kipindi kifupi cha uongozi wake na kuwa Tanzania haitamsahau.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!