Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Pinda ajitosa, akoleza mbio za urais CCM 2020
Habari za SiasaTangulizi

Pinda ajitosa, akoleza mbio za urais CCM 2020

Mizengo Pinda, Waziri Mkuu Mstaafu
Spread the love

KASI ya kusaka nafasi ya kuteuliwa na kugombea kiti cha urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), imedhihiri. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kauli za kushikana mashati zimeanza ‘kurushwa’, ambapo Mizengo Pinda, Waziri Mkuu Mstaafu amesema, utamaduni wa chama hicho unapaswa kuenziwa.

Pinda ambaye alichukua fomu ya kuwania urais 2015 na jina lake kuondolewa mapema, amesema wanaojipanga kuchukua nafasi hiyo kwenye uchaguzi mkuu ujao, wanajisumbua.

Kiongozi huyo mstaafu ametolea mfano tawala zilizopita kwamba, kwenye utawala wa Rais wa Awamu ya Kwanza, Pili, Tatu na Nne hakuwahi kuona haya yanayotokea sasa.

“Mimi nimefanya kazi na Mwl. Julis Nyerere kwa miaka minane, Mzee Mwinyi (Alhaj Ali Hassan), Mzee Mkapa (Rais Benjamin Mkapa) kwa miaka 10 lakini sikuona kinachojitokeza sasa,” amesema Pinda.

Akizungumza mbele ya wanaCCM jijini Dodoma tarehe 23 Julai 2019, wakati wa uzinduzi wa mradi wa vibanda vya biashara wa CCM.

Uzinduzi huo uliyohudhuriwa na Dk. Bashiru Ally, katibu mkuu wa chama hicho.

Pinda amesema, kulingana na utamaduni wa chama hicho, hakuna mwanachama wa CCM mwenye haki ya kugombea urais 2020.

Amesisitiza, Rais John Magufuli ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho anakaribia kumaliza kipindi chake cha kwanza cha miaka mitano, hivyo ni utamaduni apewe miaka mitano mingine.

Ni kwa kuwa, utamaduni wa CCM unampa fursa rais anayetokana na chama hicho kuhudumia vipindi viwili mfululizo.

Joto la urais 2020 kupitia CCM limekolezwa baada ya Kanal Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba kuandika barua ya kulalamikia kufafuliwa na Cryspian Musima, anayejitambulisha kuwa mtetezi wa rais.

Maelezo ndani ya barua hiyo yametafsiriwa kuwa, ni sehemu ya njama za kumvuruga Rais Magufuli kuteuliwa na chama hicho kugombea urais 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!