LUHAGA Mpinda, Waziri wa Mifugo na Uvuvi amelalamikia watu anaodai, wanataka kumng’oa Rais John Magufuli asigombee kwenye uchaguzi mkuu 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Malwilo, Tindabuligi jimboni kwake Kisesa, Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu, Mpina amesema watu wanaomsakama Rasi Magufuli ambaye ni mwenyekiti wa chama chao, ni wale waliokuwa na nyadhifa za juu serikalini na kwenye chama hicho.
Mpina amesema, pamoja na watu hao kupanga mikakati ya kumkwamisha ‘boss’ wake, mikakati hiyo haitafanikiwa.
Akizungumzia mikakati hiyo Mpina amesema, viongozi hao waliwahi kupewa nafasi za juu ndani ya CCM na Serikali, lakini Watanzania walishuhudia usimamizi dhaifu wa shughuli za chama na kusababisha makundi makubwa ndani ya chama hicho.
“Walanguzi na wala rushwa waliokuwa wanaiba fedha za taifa hili wamedhibitiwa, mishahara hewa ililipwa miaka nenda rudi viongozi wakawa wanaiba mishahara hewa kana kwamba hakuna mtu aliyetakiwa kuchukua hatua… leo Mheshimiwa John Magufuli amekuja, mishahara hewa yote imekuwa historia,” amesema Mpina na kuongeza:
“Uvuvi haramu ulikuwa kila kona, samaki walikuwa hakuna Taifa lenye maziwa makubwa kuliko nchi yoyote Afrika na Dunia, Taifa lenye bahari samaki tunanunua za kutoka nje. Mheshimiwa Magufuli akasema uvuvi haramu hapana, Mpina nenda pale kakomeshe uvuvi haramu, uvuvi haramu umekoma nchi hii,” amesema.
Amesema, kwa sasa Tanzania inashuhudiwa mageuzi makubwa aliyoyafanya Rais Magufuli katika kipindi kifupi cha uongozi wake na kuwa Tanzania haitamsahau.
Leave a comment