Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wafugaji washauriwa kutumia hospitali ya mifugo SUA
Habari Mchanganyiko

Wafugaji washauriwa kutumia hospitali ya mifugo SUA

Spread the love

WAFUGAJI wa mifugo mbalimbali nchini wameshauriwa kutumia hospitali ya Rufaa ya Magonjwa ya Mifugo Tanzania iliyopo Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kuwatibu wanyama wanapoumwa ili kuweza kunusuru uhai wao. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Akizungumza kwenye ziara ya baraza la SUA leo tarehe 27 Juni, 2019, Kaimu Rasi wa ndaki ya tiba ya mifugo, Prof. Amandus Muhairwa amesema, hospitali hiyo kwa sasa ina mashine ya Xray mpya, Ultrasound ambayo ni ya rangi pamoja na kuona namna ya kuboresha mashine za ganzi zenye gesi.

Prof. Muhairwa alisema kwa sasa wanasubiri kupata mfadhili wa kusaidia kuendeleza kutoa huduma nzuri zaidi.

Aidha alisema kwa sasa wanautaratibu wa kwenda kuwasaidia wagonjwa wa nje ambao ni wanyama wakubwa wakiwemo ng’ombe kufuatia kutokuwa na eneo kubwa lililoandaliwa kwa ajili yao kwa upasuaji na magonjwa mengine.

Pia alisema, hospitali hiyo hupokea wanyama wanaoumwa hata kutoka katika hifadhi za wanyama nchini na nje yanchi na kutoa huduma za matibabu kwa gharama zinazostahili.

Naye Mkuu wa idara ya upasuaji na uzalishaji wanyama kutoka SUA, Dk. Modesta Makungu aliwashauri wafugaji wanyama wa nyumbani kama mbwa wanaozaa hovyo mitaani kuona haja ya kuwapeleka kufanya upasuaji na kuondoa kizazi.

Dk. Makungu alisema kwa sasa wanafanya oparesheni mbalimbali ikiwemo ya kuondoa kizazi kwa wanyama kabla hawajaanza kuzaa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!