October 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CUF wacharuka kufukuzwa Wenyeviti wake

Spread the love

UONGOZI wa Chama cha Wananchi CUF wameanza kutafuta mwarobaini wa kuwarejesha wenyeviti sita wa Wilaya ya Chemba, Dodoma pamoja na mikoa mingine walioondolewa kwa amri ya wakuu wa wilaya. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Uongozi huo ukiongozwa na Mratibu wa Makamu Mwenyekiti CUF Tanzania Bara, Rajabu Mbalamwezi ambaye alifanya kikao na wananchi wa wilaya hiyo alisema kitendo kilichofanywa na mkuu wa Wilaya Chemba, Salmon Odunga pamoja na wakuu wengine wa wilaya ni makosa kisheria. 

Mbalamwezi katika kikao hicho amesema CUF kwa sasa imetangaza kuwarejesha wenyeviti wote wa vijiji walioondolewa kwa amri ya wakuu wa wilaya.

“Wakuu wa wilaya wamekuwa wakiitisha mkutano wa hadhara na kutengeneza makosa feki na kuwaondoa wenyeviti wa Miranda sasa CUF imetangaza kuwarejesha wote walioondolewa na hilo ni nchi nzima.

“Haiwezekani Mkuu wa wilaya anaamka na maamuzi yake na ikumbukwe kuwa hao wenyeviti wamepigiwa kura wamechaguliwa na wananchi kwa hali hiyo wenyeviti wanatakiwa kuheshimiwa,” amesema Mbalamwezi.

Hivi  karibuni wakuu wa wilaya walikuwa wakitumia mikutano kwa kuwasimamisha wenyeviti wa vijiji ambao wanatokana na vyama vya upinzani.

error: Content is protected !!