Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Viongozi wa Serikali wawalazikisha wapinzani kurudisha kadi
Habari za SiasaTangulizi

Viongozi wa Serikali wawalazikisha wapinzani kurudisha kadi

Spread the love

WANACHAMA wa vyama vya upinzani katika kata mbalimbali wilayani Chemba, Dodoma wamelalamikia vitendo vya watendaji wa kata kuwalazimisha kurudisha kadi za vyama vyao na kuchukua kadi za CCM. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Wanachama hao wametoa malalamiko yao katika kikao cha ndani kilichoitishwa na Mratibu wa Makamu Mwenyekiti CUF Tanzania Bara, Rajabu Mbalamwezi,wakati wa ziara yake ya kujitambulisha kwa wanachama na viongozi wa CUF Wilaya ya Chemba pamoja na kusikiliza kero zao.

Wanachama hao wa CUF wilaya ya Chemba walisema kuwa wamekuwa wakilazimishwa na watendaji kata, vijiji na vitongoji kurejesha kadi zao na kujiunga na CCM.

Mmoja wa wanachama ambao wamelalamikia jambo hilo ni pamoja na Mohamed Kambarehe (CUF) amesema viongozi wa kata wamekuwa wakiwalazimisha kurejesha kadi za vyama vyao na kujiunga na CCM.

“Mimi ni mwanachama wa CUF kwa muda mrefu na nimekuwa nafanya usafi katika soko la Kata ya Soya wilaya ya Chemba mkoani Dodoma pamoja na kusimamia usafi wa choo katika soko hilo.

“Lakini cha kushangaza viongozi wa kata akiwemo Kaimu Mwenyekiti wa Kata ya Soya wilaya ya Chemba, Zuhura Kova aliniita na kuaniambia nirejeshe kadi ya CUF na nichukue ya CCM na nisipofanya hivyo nitasitishiwa kazi za kufanya usafi sokoni na kusimamia soko.

“Niliona kama jambo la utani lakini niligoma kurejesha kadi nikaitwa tena na huyo na kusema uongozi wa kata unanihitaji nilipoenda ndipo niliambiwa nirejeshe kadi ili niendelee na shughuli lakini kutokana na umasikini niliwapa kadi ya CUF lakini hawakunipa ya CCM, wala kunipa nafasi ya kuendelea na kazi yangu badala yake waliniambia nisiendelee na nikiendelea nitawekwa ndani,” amejieleza Kambarehe.

Wanachama wengine walisema kuwa wamekuwa wakitishiwa kuwekwa ndani na watendani pale watakapoendelea kuwa wanachama wa upinzani na badala yake wajiunge na CCM.

Alipotafutwa Kaimu Mwenyekiti wa Kata ya Soya wilaya Chemba Mkoani Dodoma, Zuhura Kova ili aelezee kama tuhuma hizo ni za kweli alisema siyo kweli lakini Kambarahe amesimamishwa kufanga usafi sokoni na usimamizi wa usafi wa choo kwa kuwa muda wake umeisha na alitakiwa kujaza fomu upya.

Alipoulizwa ni lini utaratibu wa kujaza fomu na kuomba hiyo kazi na mwanzoni walikuwa wamitumia utaratibu gani, amesema kuwa walikuwa wakitumia utaratibu wa kuteua kwa kutumia vikao.

Alipoombwa kuonesha muktasari ya vikao vya utafiti, Kova amesema utaratibu ulikuwa hivyo hivyo huyo kijana itakiwa kujaza fomu na kama hakujaza fomu ni bahati mbaya kwake.

Naye Mratibu wa Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara CUF, Rajabu Mbalamwezi katika kikao hicho mesema kuwa CUF inalaani vitendo vya viongozi wa serikali kuingilia mambo ya siasa na kuwalazimisha wapinzani kujiondoa kwenye vyama vyao na kujiunga na CCM.

Amesema CUF haitakuwa tayari kuona wanachama wake wakionewa na badala yake watapambana hadi hatua ya mwisho huku hakitoa onyo kwa watendani ambao wamekuwa wakitoa vitisho kwa viongozi au wanachama wa CUF na upinzani kwa ujumla

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

error: Content is protected !!