Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Tuhuma za rushwa: Ofisa TRA, Polisi wapandishwa kizimbani
Habari Mchanganyiko

Tuhuma za rushwa: Ofisa TRA, Polisi wapandishwa kizimbani

Spread the love

CHARITY Ngwala (28), Ofisa Msaidizi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), H 4810 PC Ramadhani Uweza (28) na H 48 86 PC Simon Sugu (26) ambao ni askari polisi wa Kituo cha Polisi cha Osterbay, wamepandishwa kizimbani leo tarehe 10 Juni 2019. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Maofisa hao wamepandishwa kizimbani na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kuomba rushwa ya Sh. 2 Milioni.

Akisoma hati ya mashtaka, wakili wa  serikali kutoka Takukuru, Sofia Ngula amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa, tarehe 29 Oktoba 2016 Kimara Mwisho, jijini Dar es Salaam washtakiwa hao walishawishi rushwa ya Sh. 2 Milioni kutoka kwa mfanyabiashara wa Karikaoo, Ramadhani Ntunzwe.

Maofisa hao walimshawishi Ntunzwe ili waachie mizigo yake kwa madai kuwa, alifanya udanganyifu wa bidhaa alizonazo na hivyo kuathiri ukadiriaji wa kodi, kazi ambayo ni ya mwajiriwa wake.

Hata hivyo, washtakiwa wamekana shtaka hilo na wameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti yaliyowekwa na mahakama ambapo wametakiwa kuwa na mdhamini moja mwenye kitambulisho, atakayesaini bondi ya Sh. 5 milioni.

Kwa mujibu wa upanda wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo haujakamilika na wako katika hatua za mwisho kukamilisha. Kesi imeahirishwa hadi tarehe 10 Julai mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

error: Content is protected !!