Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Gesi asilia kusambazwa, kupunguza matumizi ya kuni, mkaa
Habari Mchanganyiko

Gesi asilia kusambazwa, kupunguza matumizi ya kuni, mkaa

Kituo cha kupokea gesi asilia cha Kinyerezi, Dar es Salaam
Spread the love

SUBIRA Mgalu, Naibu Waziri wa Nishati amsema, serikali imeanza kutekeleza mradi wa kusambaza gesi asilia katika miji ya Mtwara, Lindi, Pwani na Dar es Salaam ili kupunguza matumizi ya kuni na mkaa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Mgalu ametoa kauli hiyo leo tarehe 15 Mei 2019 bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Kibiti, Ally Ungando (CCM).

Katika swali lake lenye vipengele (a) na (b) Ungando alitaka kujua, wananchi wanaoishi katika Jimbo la Kibiti hutumia nishati ya kuni kwa matumizi ya nyumbani, shuleni, gerezani hivyo husababisha uharibifu mkubwa wa mazingira kwa kukata miti hovyo.

“Je, serikali ina mkakati gani wa kupeleka nishati mbadala? Na je, njia gani ya nishati itakayotumika badala ya kuni na mkaa?” ameuliza Ungando.

Akijibu swali hilo Naibu Mgalu amesema, serikali kupitia sera ya Taifa ya nishati ya mwaka 2015, imetoa mwongozo wa kuboresha maisha ya wananchi kwa matumizi bora ya nishati kupitia teknolojia ya kisasa badala ya kuni na mkaa.

Aidha amesema, serikali imekuwa ikichukuwa jitihada za makusudi kuendeleza vyanzo mbalimbali vya nishati ili kuongeza mchango wa nishati mbadala katika upatikanaji wa nishati nchini.

“Katika kipindi cha muda wa kati kuanzia mwaka 2015 hadi 2020, serikali inatekeleza miradi ya kuzalisha umeme kupitia vyanzo vya gharama nafuu vya maji na gesi ikiwa ni mkakati wa kuwawezesha wananchi kumudu kutumia nishati ya umeme kwa gharama nafuu, kwa ajili ya kupikia badala ya kuni na mkaa.

“Kwa kuwa sehemu ya kuni na mkaa unaotumika katika Jiji la Dar es Salaam huzalishwa katika Wilaya ya Kibiti, hatua ya kwanza kutumia gesi asilia kwa kupikia itapunguza uharibifu mkubwa wa mazingira kupitia ukataji miti hovyo kwa matumizi ya kuni na mkaa,” amesema Mgalu.

Hata hivyo katika hatua nyingine amesema tarehe 18 Mei 2018, serikali kupitia Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) ilisaini mkataba na Kampuni ya Mihan gas kwa ajili ya kusambaza vifaa vya kupikia mitungi ya gesi na majiko kwa watumishi wa Umma na wananchi wengine na kuwa, mpango huo unalenga kupunguza matumizi ya mkaa na kuni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

error: Content is protected !!