December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Shahidi kesi ya Mbowe: Nilipigwa jiwe, nikazimia

Freeman Mbowe na viongozi wa Chadema wakiwa mahakamani Kisutu

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam imeendelea kusikiliza kesi namba 112 ya uchochezi, inayowakabili viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Leo tarehe 15 Mei 2019, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, upande wa Jamhuri umewasilisha shahidi wake wa tatu.

Wakili wa Jamhuri kwenye kesi hiyo ni Faraja Nchimbi, Wankyo Simon, Paul Kadushi ambapo mawakili upande wa washtakiwa ni Profesa Safari, Mwasipu, Peter Kibatala, Mallya, Gipson Mbatata, Edson.

Koplo Rahim Msangi (48), Ofisa wa Polisi ndio shahidi wa Jamhuri. Kituo cha kazi, Polisi Osterbay. Amehojiwa na wakili wa serikali Wankyo Simon kama ifuatavyo:-

Wakili: Umekuwa kazini kuanzia lini?

Shahidi: Kuanzia 2017 hadi sasa 2019

Wakili: Iambie mahakama kabla ya Osterbay ulikuwa wapi?

Shahidi: Nilikuwa Kituo cha Polisi cha Kutuliza Ghasia Mkoa Dar es Salaam

Wakili: Kituo cha Polisi Osterbay kipo mahala gani?

Shahidi: Kipo Kinondoni, Dar es Salaam

Wakili: Iambie mahakama, hapo Osterbay unatekeleza  majukumu gani kila siku?

Shahidi: Kulinda raia na mali zao, kusimamia usalama wa raia

Wakili: Jukumu jengine?

Shahidi: Kusindikiza misafara ya kiserikali

Wakili: Jengine kama lipo?

Shahidi: Kupeleleza na kukamata makosa

Wakili: Iambie mahamakama tarehe 16 Februari 2018 ulikuwa wapi?

Shahidi: Niliingia kazi Polisi Osterbay majira ya saa 12 asubuhi.

Wakili: Ni kitu gani ulipangiwa kukifanya?

Shahidi: Nilipangiwa kufanya doria maeneo ya Wilaya ya Kinondoni

Wakili: Ifafananulie mahakama, ukisema Wilaya ya Kinondoni unamaanisha nini na kuhusiana na hiyi doria?

Shahidi: Gari tunayopangiwa ni kufanya doria kuzunguka maeneo ya Kinondoni.

Wakili: Ulikuwa na kina nani?

Shahidi: Nilikuwa na askari PC Issa, PC Serenga, WP Hadija, PC Khalifa

Wakili: Na mwengine unaowakumbuka au isaidie mahakama mlikuwa askari wangapi?

Shahidi: Sita

Wakili: Walikuwa wanaongozwa na nani?

Shahidi: Inspeta Mohmede

Wakili: Wewe ulikuwa na jukumu gani?

Shahidi: Nilikuwa kamanda wa askari wa doria hiyo

Wakili: Iambie mahakama ukiwa kwenye mizunguko yenu majira ya saa 11 taarifa ipi mliipokea?

Shahidi: Majira ya saa 11 nilikuwa maeneo ya Mwenge.

Wakili: Ukiwa maeneo hayo nini kilitokea?

Shahidi: Tulipanda gari maeneo ya ITV tukapaki gari na Afande Mohammed Mzelengi tukashuka, tukawa tunajadiliana twende maeneo yenyu uhalifu.

Iliingia Radio Call iliyokuwa kutoka kwa OCD Afande Dotto. OCD wa Wiliya Kinondoni kuwa alipokea barua na kupokea maelekezo kuwa tuondokea pale tuelekee maeneo ya Mwananyamara Buibui.

Wakili; Sasa iambie mahakama wewe maelekezo hayo uliyapataje?

Shahidi: Niliyapata kupitia Afande Mzelengi

Wakili: Yalikuwa ni ya kufanya nini?

Shahidi: Alitujulisha sisi kuwa, tunahitajika tuondoke pale Mwenge tuelekee Mwananyamara viwanja vya Buibui, ambako kuna mkutano wa Chadema ambao viongozi wao, walikuwa wakipanda kwenye majukwaa na kutoa maneno ya uchochezi.

Wakili: Aliwataka mkafanye nini?

Shahidi: Kwa ajili ya kuongeza nguvu

Wakili: Nyie mlichukua hatua gani?

Shahidi: Baada ya kutoka Mwenge hadi Buibui, afande Mzerengi alienda moja moja kwa hadi kwa afande Dotto

Wakili: Ilikuwa muda gani?

Shahidi: Tulifika Saa 11 na robo na kuendelea

Wakili: Kitu gani mlikifanya?

Shahidi: Baada ya kufika, tulipata maelekezo yaliyotolewa na OCD kuwa, mkutano unaendelea lakini kuna maneno yanayoashiria uvunjifu wa amani

Wakili: Iambie mahakama, ni kitu gani mlikifanya pale?

Shahidi: Baada kufika na kuwapanga askari, niliona mgombea wa Chadema akinadi sera zake

Wakili: Unaweza kuiambia mahakama, kitu gani ulikiona au ulikisikia?

Shahidi: Sikuweza kuelewa anaongea nini kwasababu nilikuwa kati napanga askari. Baada ya hapo nilimshuhudia Mbowe amechukua maiki kutoka kwa mgombea alitoa maelekezo.
Alitoa maelekezo ya…

Wakili: Hebu tufafanulie vizuri, hakimu anaweka rekodi vuzuri.
Ni kitu gani unasema kwa ufasaha Mwenyekiti Mbowe.

Shahidi: Baada ya kupokea maiki, alitoa tamko la kuwasindikiza viongozi

Wakili: Wafanye nini?

Shahidi: Kwamba lazima tuandamane kwenda kwa mkurugenzi wa Manspaa ya Kinondoni

Wakili: Kwenda kufanya nini?

Shahidi: Kuchukua barua zao

Wakili: Baada ya tamko hilo, ni kitu gani unakumbuka kilitokea?

Shahidi: Baada ya kuwashawishi viongozi na raia ambao ni wafuasi kwamba, ni lazima twende kwa mkurugenzi. Wakati huo watu waliokuwa uwanjani ni wengi na alitoa rai kwamba, waandamane na kilichofanyika alirejesha maiki na kushuka kwenye jukwaa akiwa yeye na viongozi na wafuasi wa Chadema.

Wakili: Sasa Koplo Rahimu, iambie mahakama hali ya uwanja wa Buibui wakati huo ilikuwaje?

Shahidi: Hali kwa ujumla viwanja vya Buibui wananchi walikuwa wanahasira ambazo zilisababishwa na uongozi uliokuwepo ambao ni Mh Mbowe.

Wakili: Pengine walikuwa kwenye hali gani?

Shahidi: Walikuwa kwenye taharuki na kutamka maneno ya kuashiria uvunjifu wa amani

Wakili: Waliokuwepo kwenye eneo hilo, walikuwa na hasira na kutoa kauli zinazoashira uvinjifu wa amani. Labda kwa uchache maneno uliyasikia yaliashiria uvunjifu wa Amani?

Shahidi: Walitamka hatuogopi, hatutishiki tutaandamana hadi kieleweke

Wakili: Shahidi kwa ufafanuzi ulisema kuna viongozi walishuka, kwa ufafanuzi viongozi walioteremka unaowakumbuka?

Shahidi: Namkumbuka Mwenyekiti wa Chadema, Mbowe, Halima Mdee, wengine siwafahamu kwa majina bali ninawafahamu kwa sura kwasababu niliwaona eneo la tukio.

Wakili: Pengine iambie mahakama, hao ambao unasema huwafahamu kwa majina na walikuwepo unaweza kuiambia mahamama wapo wapi?

Shahidi: Katika mahakama hii hao hapo waliokaa mbele ya….

Wakili: Sasa shahidi Rahimu utainoesha mahakama watu hao ambao unasema uliwatambua kwa majina yao na wengine ulikuwa huwajui majina yao. Tunaiomba mahakama shahidi akatuoneshe hao anasema anawakumbuka kwa sura na wengine hawajui kwa majina. Tuendelele.

Shahidi: Huyu hapa mwenyekiti na huyu hapa Halima Mdee- aliwashika.

Wakili: Na wengine uliosema uliwaona

Shahidi: Akawaonesha Dk. Mashinji Vicent akasema sio mgeni kwa jina

Hakimu Simba: Hayo uliyoyasema mwisho sio yale aliyokuongoza

Shahidi: Amemwonesha John Mnyika, Ester Matiko kwa mkono wa kurusha

Hakimu Simba: Usiwapige waguse tu

Shahidi: Akamaliza, aliwagusa saba na kuacha wawili

Wakili: Mjadala watuhumiwa wanadai hajawagusa wawili.

Hakimu Simba: Hata mimi nimeona hajawagusa.

Mjadala kidogo kimya kimya

Hakimu Simba: tuendelee

Wakili: Iambie mahakama, walipotoka hapo Buibui walielekea wapi?

Shahidi: Ukisema walielekea wapi, unataka majibu unayota wewe.

Wakili: Sawa Mhe nini kilitokea?

Shahidi: Niliowataja mwenyekiti na niliowagusa walishikana mikono na kuongoza maandamano kupitia njia ya Mwananyamara kuelekea Studio. Walipofika Studio waliingia Barabara ya Kawawa uelekeo wa kwenda kwenye Ofisi za Mkurugenzi wa Kinondoni ambapo ofisi zake zipo Magomeni.

Wakili: Umeongea maneno umati, iambie mahakama umati kwa makadirio ni watu wangapi?

Shahidi: Kwa makadirio kuanzia watu 400 hadi 700

Wakili: Iambie mahakama kwenye yale maandanano watu walikuwa wangapi?

Shahidi: Kuanzia watu 400 hadi 700

Wakili: Baada ya watu hao kuondoka, mlifanya kitu gani?

Shahidi: Wakati tukiwa viwanja Buibui kulingana na idadi ya watu, hatukuweza kutoka muda uleule, tulibaki maeneo yale kwanza

Wakili: Ni kitu gani kilifuatia?

Shahidi: Baada mwenyekiti kutoka na watu wake,
punde afande Ngerenji aliitwa kwenye Radio call. Alituambia ameitwa na Ofisa Operesheni wa Mkoa

Wakili: Anaitwa nani?

Shahidi:  Ngichi. Alituambia tuelekee Mkwajuni maandamano yanaendelea.

Wakili: Sasa mlifanya kitu gani?

Shahidi: Tulijiondoa maeneo ya Buibui kupitia pembezoni na kuelekea Mkwajuni

Wakili: Nini kiliwafanya mpite pembezoni?

Shahidi: Barabara kuu ilikuwa imefungwa, gari zilikuwa hazitembei wafuasi walitanda

Wakili: Mlifika saa ngapi?

Shahidi: Saa 12 kasoro

Wakili: Mlipewa maelekezo gani?

Shahidi: Tulikwenda maeneo ya Mkwajuni kwenye mteremko wa kwenda Magomeni na tukamuona afande Ngichi yupo pale.

Wakili: Nini kiliendelea baada kufika hapo?

Shahidi: Baada ya kufika alipo Ofisa Operesheni wa Mkoa, tuliamuriwa kushuka kwenye magari. Baada ya kushuka kwenye magari tuliona waandamanaji walishafika kwenye Kituo cha Mwendokaso wakiimbia hatuogopi, mtatuua. Niliwaona kwenye Mwendokasi kwa macho yangu wakimbia mtatuua, wanarusha mawe, wanarusha chupa

Wakili: Hali ya watu waliondamana ilikuwaje?

Shahidi: Hali ya maandamano ilikuwa hali ya hatari. Walikuwa wanarusha mawe na wengine walikuwa wamevaa mizura kufunika uso yaani huwezi kumuona huyo nani

Wakili: Nini kiliendelea?

Shahidi: Afande Operesheni wa Mkoa alitoa ilani akisema, Ilani Ilani watu mnaoandamana hayo maandamani sio sahihi, mtawanyike mara tatu la sivyo tutatumia nguvu.

Wakili: Baada ya hapo nini kilijitokeza?

Shahidi: Baada ya kukaidi ilani iliyotolewa na Ofisa Operesheni, tulipigwa mawe, afande akatoa amri ya kupigwa mabomu.

Wakili: Nataka uiambie mahakama, ilani ilitolewa na Afande Ngichi, nini kiliafikiwa kwa waandamanaji?

Shahidi: Waandamani waligoma kusitisha maandamano. Baada ya waandamanaji kutokutii amri ya polisi, afande Ngichi aliamuru kupigwa mabomu

Wakili: Muitikio wa waandamaji ulikuaje?

Shahidi: Walisema kuwa, mtatuua na walikuwa wakisema wanakwenda kwa mkurugenzi, wanakwenda kuchukua barua zao kwa ajili ya The Peoples.

Wakili: Hao waandamanaji walioshika mawe, chupa baada ya Ilan kutolewa ni kitu gani walifanya?

Shahidi: Walitumia mawe, chupa za maji kutushambulia sisi askari tuliokuwepo eneo hilo

Wakili: Wakati huo viongozi wa Chadema walikuwa wapi?

Shahidi: Walikuwa mbele ya waandamanaji kuhamasisha kuendelea mbele wasirudi nyuma

Wakili: Sasa baada ya Ilani kutolewa, ulisema mawe yalirushwa pengine nini kilitokea?

Shahidi: Afande Ngichi alitoa oda ya kupiga mabomu

Wakili: Kwa lengo gani?

Shahidi: Kwa lengo la kuwatanya waandamanaji

Wakili: Ifafanululie mahakama, nini kiliendelea baada ya mabomu?

Shahidi: Baada ya kupiga mabomu, tulisimama upande ambao upepo unarudisha moshi

Wakili: Upepo ulikuwa ukiendelea upande gani?

Shahidi: Upande wa Magomeni tuliokuwa tumesimama

Wakili: Ule upepo ulikuwa ukiwafuata kina nani?

Shahidi: Upepe uliturejea sisi askari

Wakili: Nini kiliendelea?

Shahidi: Wakati upepo ulipokuwa ukiendelea nini kilifuatia?

Wakili: Mimi nilipigwa jiwe na sikujua nini kiliendelea mpaka nikajikuta Hospital ya Polisi

Wakili: Jiwe lilitokea wapi?

Shahidi: Jiwe lilitokea upande wa waandamanaji na sikujua aliyepiga mawe

Wakili: Ulijuaje kama kilichokupiga ni jiwe?

Shahidi: Nilijua ni jiwe kwasababu muda wote ndio waliyokuwa waliyatumia kuturusha

Wakili: Ulisema umepelekwa Hospital ya Polisi, wapi?

Shahidi: Hospitali ya Polisi, Kilwa Road

Wakili: Iambie mahakama ukiwa pale hospitali ulipozinduka ulibaini nini kuhusiana na kupigwa kwako?

Shahidi: Baada ya kuwa na kumbukumbu, nilikumbuka nilikuwa nina silaha SMG.

Wakili: Baada ya kukumbuka kuwa ulikuwa na silaha, nini kilifuatiwa?

Shahidi: Sikuwa na silaha, niliwekewa dripu

Wakili: Nini kilifuatia?

Shahidi: Baadaye si muda mrefu alikuja Afande Mzirengi

Wakili: Ilikuwa lini?

Shahidi: Kesho tarehe 17. Nilimuliza afande Mzirengi nilikuwa na silaha, silaha yangu ipo wapi?

Wakili: Aliniambia silaha ipo Polisi Osterbay

Shahidi: Baada ya kutumia silaha, ilichukuliwa na askari wenzangu kituo cha Polisi Osterbay

Wakili: Ulipopata fahama uliweza kugundua nini kilichokufanya uputezee fahamu?

Shahidi: Niligundua nilipigwa jiwe kwenye maandamano nilipigwa jiwe la shingo.

Wakili: Sasa ulifika Hospitali na kikawaida kuna nyaraka unayofanya utibiwe…kama kuna uthibitisho wowote ambao unaweza kuonesha mahakama kama kweli ulitibiwa

Shahidi: Baada ya kupigwa nilipewa PF3

Wakili: Labda ukionesha hiyo PF3 utaweza kuitambua? Ni kitu gani kitachokufanya uitambue?

Shahidi: PF3 inakuwa namba zangu za kijeshi. Namba zangu ni E6979 Kolpo Rahimu

Wakili: Naomba nimuoneshe shahidi nyaraka. Wakili amemuonesha hakimu PF3

Wakili: Unapenda mahakama iifanye nini?

Shahidi: Naomba mahakama iipokee

Wakili: Naiomba mahakama kuipokea nyaraka hii na kuitambua kuwa shahidi ameitambua

Upande wa utetezi wameikagua PF3 na kueleza kuwa, hawana pingamizi nao.

Wakili: Sasa shahidi ulipokuwa viwanja vya Buibui, uliwaona viongozi iambie mahakama ulikuwa umbali kiasi gani ukiwa eneo la Buibui?

Shahidi: Nilikuwa mzunguko wa uwanja kwa wale raia kwa hiyo wale raia walikuwa ndani ya uwanja. Mahala nilipokuwa nimesimama ni kama mita 15.

Wakili: Kitu gani kilichokusaidia kuwatambua kuwa yule ni Fulani?

Shahidi: Niliowaona kwa macho na wengine kuwafahamu

Wakili: Majira hayo hali ya mwanga ilikuaje?

Shahidi: Hali ya mwanga ilikuwa ya kawaida kiasi ambacho niliweza kuwaona..

Wakili: Hawa wengine ambao ulisema ni huwafahamu kwa majina ni kwa muda gani uliwajua kama ni viongozi wa Chadema?

Shahidi: Niliwajua kuwa ni viongozi wa Chadema niliwaona kwenye vyombo vya habari, kwenye magezeti tunawaona

Wakili: Hawa vingozi ulikuwa nao umbali gani?

Shahidi: Eneo la Mkwajuni kuna juu wengine walikuwa mbele yetu wakiturushia mawe.

Wakili: Nataka uiambie mahakama wale viongozi wa uliosema unawajua na wengine huwajui kwa majina, ulikuwa nao umbali gani?

Shahidi: Makadirio ni mita 20

Wakili: Hali ya mwanga ilikuwaje?

Shahidi: Ilikuwa ya kawaida na nilikuwa naona kama navyoona sasa hivi.

Wakili: Ifafanulie mahakamma mwanga ulikuaje?

Shahidi: Ilikuwa ni mchana
Wakili: Kwani mwanga ulikujae?

Shahidi: Ulikuwa naweza kuona

Upande wa serikali umemaliza kumuongoza shahidi.

Itaendelea

error: Content is protected !!