November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Viongozi wa dini kupambana na Saratani Mlango wa Kizazi

Dk. Faustin Ndungulile

Spread the love

VIONGOZI wa dini kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamie, Jinsia, Wazee na Watoto wanakusudia kufanya kongamano la pamoja kujadili uanzishwaji wa chanjo ya kukinga Saratani ya Mlango wa Kizazi. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Mkurugenzi wa maandalizi ya maombi hayo ya kitaifa yatayofanyika jijini Dodoma kuanzia 22 hadi 30 Juni mwaka huu, Askofu Mkuu wa Kanisa la Endtime Haverst Tanzania Dk. Elia Mauza amesema, maandalizi hayo yamefikia asilimia 100.

Aidha Dk. Mauza ambaye pia ni Kaimu Mratibu wa Engenger Health amesema kuwa, viongozi wa dini kwa kushirikiana na wadau wa afya, wanalenga kuhakikisha wanashirikiana ili kutatua matatizo ya afya.

Amesema kuwa, wizara hiyo kwa kushirimiana na wadau wa Engenger Health, wameandaa kikao maalum cha kuongea na viongozi wa dini pamoja na waandishi wa habari ili kujadili masuala ya chanjo hususani chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi.

Dk. Mauza amesema, wizara kupitia mpango wa Taifa imepanga kufanya kikao hicho kesho tarehe 16 Mei 2019 katika ukumbi wa mikutano katika Hotel ya Morena, Jijini Dodoma.

Amesema, lengo la kikao hicho ni kujadili mafanikio na changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa huduma ya chanjo ya kukinga mabinti dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi tangu ianzishwe Aprili mwaka jana.

“Baada ya kuanzishwa chanjo hii mwitikio ulikuwa ni mkubwa,lakini baada ya kuanzishwa kumekuwa na kiwango cha chini kwa dozi ya pili” amesema Dk. Mauza.

error: Content is protected !!