Tuesday , 30 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Lukuvi ateua wenyeviti 20 wa mabaraza ya ardhi
Habari Mchanganyiko

Lukuvi ateua wenyeviti 20 wa mabaraza ya ardhi

Spread the love

WILLIAM Lukuvi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amewateua wenyeviti 20 wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya kwa kipindi cha miaka mitatu. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Akizungunza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa bunge leo tarehe 7 Mei 2019 amesema, kwa mamlaka aliyonayo, yanampa nafasi ya kuteua wenyeviti hao pale anapoona inafaa.

“Kwa Mamlaka niliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 25(1) cha sheria ya mahakama za utatuzi wa migogoro ya ardhi, sura 216, nimewateua wenyeviti 20 wa mabaraza ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ya Wilaya kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Aprili moja mwaka huu,” amesema Lukuvi.

Amewataja wateule hao kuwa ni Rajabu Mnyukwa, Edward Muhina, Nadhiru Ngukulike, Rebeca Mjanja, Hussein Lukeha, Augustine Lugome, Baraka Shuma, Tendai Chinolo, Mangeti Sangiwa, Jackson Kanyerinyeri, Jacob Kabisa, Ntumengwa Moses, Justine Lwezaura, Jesca Mugalu, Regularly Mtei, Jimson Mwankenja, Bahati Ndambo, Richard Mmbando, Felix Rutajangulwa na Ngasa Masunga.

Akizungumzia kushughulikia migogoro ya ardhi Lukuvi alisema wizara imeunda mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya 97 kwajili ya kushughulikia utatuzi wa migogoro ya ardhi kwa mujibu wa sheria ya mahakama na utatuzi wa migogoro ya ardhi sura 216.

“Nimekuwa nikipokea tuhuma kuhusu utendaji wa wenyeviti wa mabaraza  ya ardhi na nyumba ya wilaya hususani mabaraza ya wilaya ya Karagwe na Kibaha.

“Kwa mamlaka niliyonayo namuagiza Katibu mkuu kuanzia leo, kuwasimamisha kazi wafuatao ilikupisha uchunguzi.

“Waliosimamishwa ni Rugate Assey mwenyekiti wa baraza la ardhi na nyumba wilaya ya Karagwe na Jerome Njiwa Mwenyekiti wa baraza la ardhi na nyumba wilaya ya Kibaha,” alisema Lukuvi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

7 wafa Ulanga, mbunge alia kutelekezwa na mawaziri, Tanroad

Spread the loveWatoto saba wamepoteza maisha na zaidi ya kaya 70 kukosa...

Habari Mchanganyiko

Bil 12.4 zimetumika ujenzi wa miradi wilaya ya Momba

Spread the love MKUU wa wilaya ya Momba mkoani Songwe Kennan Kihongosi...

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

Habari Mchanganyiko

NBC yapata tuzo ya mwezeshaji bora wa mikopo serikali Afrika

Spread the loveBenki ya NBC imepata tuzo ya Mwezeshaji Bora wa Pamoja...

error: Content is protected !!