Monday , 22 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Bila ya Mzee Mengi labda ningekuwa kipofu – Kubenea
Habari Mchanganyiko

Bila ya Mzee Mengi labda ningekuwa kipofu – Kubenea

Spread the love

MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea amesema, hatosahau msaada wa hali na mali aliopata kutoka kwa Marehemu Dk. Reginald Abraham Mengi, alipomwagiwa tindikali mwaka 2008 na watu wasiojulikana. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Ametoa kauli hiyo leo tarehe 7 Mei 2019, wakati wa kuuaga mwili wa Dk. Mengi ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kampuni zilizo chini ya IPP kwenye viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.

Amesema, bila msaada wa Dk. Mengi, pengine kwa sasa angekuwa kipofu kutokana na tukio hilo la kumwagiwa tindikali katika macho.

“Mzee Mengi alikuwa kama mzazi, kaka, rafiki na kiongozi aliyenibeba kama mithiri ya mtoto wake wa kumzaa. Nakumbuka mwaka 2008 nilipopata majanga ya kumwagiwa aside, alijitolea kunifariji na kunipeleka nje kunitibia kwa gharama zake bila kujali, bila yeye na wengine pengine ningekuwa kipofu,” amesema Kubenea.

Kubenea alisema hayo baada ya kuwasilisha ujumbe wa Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema-Taifa na Mbunge wa Hai ambaye ameshindwa kuhudhuria shughuli hiyo.

Akiwasilisha salamu za Mbowe, Kubenea amesema kuwa Mbowe ameeleza kuwa, alikuwa na wakizungumza na Dk. Mengi masuala mbalimbali ya siasa na biashara.

“Mara nyingi tulizungumza na kubishana kuhusu siasa, maisha na biashara, nilitambua magumu uliyopitia,” ameandika Mbowe kwenye ujumbe wake aliomkabidhi Kubenea kuuwasilisha.

Akizungumzia uhusiano wake (Kubenea) na Dk. Mengi, mbunge huo wa Ubungo amesema, amepata msaada mkubwa kutoka kwa mfanyabiashara huyo.

Kubenea ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hali Halisi inayochapisha Gazeti la MwanaHALISI na MwanaHALISI ONLINE akiwa na mshauri wa kampuni hiyo, Ndimara Tegambwage, mwaka 2018 walivamiwa na kushambuliwa na watu ambao mpaka sasa hawajatambulika.

Kwenye shambulizi hilo, Kubenea alimwagiwa tindikali usoni, hivyo alipelekwa India kwa matibabu zaidi huku Ndimara akikatwakatwa panga kichwani.

Akizungumza kwenye shughuli ya kuuaga mwili wa Dk. Mengi Kubenea Amesema, Dk. Mengi alijitoa kwa hali na mali akishirikiana na watu wengine, kumsafirisha nje ya nchi kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya majeraha aliyopata.

“Kweli tumepungukiwa ni kweli wanasema, mlango mmoja ukifungwa unafunguliwa mwingine lakini ukweli utabaki kuwa, hakutakuwa na Mengi wawili, niseme kwamba Mzee Mengi alikuwa chachu,” amesema Kubenea.

Aidha, Kubenea amesema, atamkumbuka Dk. Mengi kwa hulka yake ya kujali utu wa mtu bila ya kujali tofauti za kiitikadi na kidini.

Amesema, licha ya Dk. Mengi kuwa mwanachama wa CCM, lakini aliutumia utajiri wake kuvisaidia vyama vyote.

 “Mengi alikuwa mwanachama wa CCM ni ukweli kwamba, itikadi zetu halikuwa jambo la umuhimu kwake, aliamini katika maendeleo ya nchi. Alithamini utu wa mtu na si itikadi ya vyama, alitumia fedha zake kusaidia vyama vyote,” amesema Kubenea.

Amesema, ni vyema taifa na Watanzania kwa ujumla kuonesha kuguswa kwa kifo cha Dk. Mengi kwa kuyaenzi mema aliyofanya, kwani kutokufanya hivyo ni sawa na kutoguswa na kifo chake.

“Kama tunataka kumuenzi Dk. Mengi kwa dhati kuyaenzi, tusijifanye tunampenda wakati tunabaguana kwa itikadi zetu.

Niwaombe wote tulioguswa na msiba huu tuendelee kuenzi yale yote mema ambayo Mzee Mengi aliyafanya kwa watu,” amesema Kubenea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

DC ampongeza Dk. Rose Rwakatare kwa kusaidia waathirika wa mafuriko Mlimba

Spread the loveMWENYEKITI wa Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk.  Rose Rwakatare...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

Habari Mchanganyiko

DCEA yakamata kilo 767.2 za dawa za kulevya, 21 mbaroni

Spread the love  MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya...

error: Content is protected !!