WILLIAM Lukuvi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amewateua wenyeviti 20 wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya kwa kipindi cha miaka mitatu. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Akizungunza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa bunge leo tarehe 7 Mei 2019 amesema, kwa mamlaka aliyonayo, yanampa nafasi ya kuteua wenyeviti hao pale anapoona inafaa.
“Kwa Mamlaka niliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 25(1) cha sheria ya mahakama za utatuzi wa migogoro ya ardhi, sura 216, nimewateua wenyeviti 20 wa mabaraza ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ya Wilaya kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Aprili moja mwaka huu,” amesema Lukuvi.
Amewataja wateule hao kuwa ni Rajabu Mnyukwa, Edward Muhina, Nadhiru Ngukulike, Rebeca Mjanja, Hussein Lukeha, Augustine Lugome, Baraka Shuma, Tendai Chinolo, Mangeti Sangiwa, Jackson Kanyerinyeri, Jacob Kabisa, Ntumengwa Moses, Justine Lwezaura, Jesca Mugalu, Regularly Mtei, Jimson Mwankenja, Bahati Ndambo, Richard Mmbando, Felix Rutajangulwa na Ngasa Masunga.
Akizungumzia kushughulikia migogoro ya ardhi Lukuvi alisema wizara imeunda mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya 97 kwajili ya kushughulikia utatuzi wa migogoro ya ardhi kwa mujibu wa sheria ya mahakama na utatuzi wa migogoro ya ardhi sura 216.
“Nimekuwa nikipokea tuhuma kuhusu utendaji wa wenyeviti wa mabaraza ya ardhi na nyumba ya wilaya hususani mabaraza ya wilaya ya Karagwe na Kibaha.
“Kwa mamlaka niliyonayo namuagiza Katibu mkuu kuanzia leo, kuwasimamisha kazi wafuatao ilikupisha uchunguzi.
“Waliosimamishwa ni Rugate Assey mwenyekiti wa baraza la ardhi na nyumba wilaya ya Karagwe na Jerome Njiwa Mwenyekiti wa baraza la ardhi na nyumba wilaya ya Kibaha,” alisema Lukuvi.
Leave a comment