September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polepole: Watu mashuhuri wanaokufa ni wa CCM

Spread the love

HUMPHREY Polepole, Katibu wa Itikati na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema, watu wengi mashuhuri wanaokufa huwa wanachama wa chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akitoa salamu za pole kwenye kwenye shughuli ya kuuaga mwili wa Dk. Reginald Abraham Mengi iliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam leo tarehe 7 Mei 2019, Polepole amesema CCM ina bahati ya kuwa na watu maarufu.

“Kwenye chama chetu tuna bahati, watu wote mashuhuri wanaokufa ni wana CCM, Mzee Menegi wala hakujificha, alikuwa rafiki wa Rais Magufuli (Rais John Magufuli,” amesema.

Kwenye salamu zake kwa wafiwa, Polepole amewataka kutokata tamaa na kuwa imara kama alivyokuwa Dk. Mengi.

“Tusikate tamaa, tupambane kama mtu, taasisi na taifa. Dk. Mengi ametufundisha kutafuta. Alikuwa mtu madhubuti, makini na ambaye ametuonesha kwamba, inawezekana,” amesema.

Amesema, baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ndani ya chama hicho hakukuwa sawa kidogo na kwamba, ushauri wake umesaidia kuweka mambo sawa.

Ameeleza kuwa, ni vizuri Watanzania wakaendeleza dhamira ambayo Dk. Mengi aliyoonesha kama mfano huku akisisitiza kuendelea kuwekwa vizuri mazingira ya sekta binafsi.

error: Content is protected !!