Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli atinga Kiwira kwa Mkapa, Yona
Habari za Siasa

Rais Magufuli atinga Kiwira kwa Mkapa, Yona

Mgodi wa Makaa ya mawe
Spread the love

WAKATI serikali ikiendelea kufanya mchakato kuuchukua Mgodi wa Kiwira, umekutwa na madeni hewa zaidi ya bilioni 40. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mgodi huo uliopo Rungwe, Mbeya ulizua mjadala kwa kudaiwa kumilikiwa na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, Mama Anna Mkapa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona.

Kwa mujibu wa Dotto Biteko, Waziri wa Madini mbele ya Rais John Magufuli leo tarehe 29 Aprili 2019, serikali imebaini kuwepo kwa deni hewa zaidi ya bilioni 40.

Biteko amesema, kabla ya Serikali ya Awamu ya Tano kufanya uhakiki wa deni la mgodi huo, deni la mgodi huo lilikuwa Sh. 46 bilioni huku wanaodai wakiwa 1862, na kwamba, baada ya uhakiki huo, ilibainika deni halisi kuwa Sh. 1.24 bilioni, na idadi ya wanaodai ni 862.

“Toka serikali yako ilivyoingia madarakani, ulifanya kazi ya kusimamia na deni ili mgodi huu ufanye kazi kwa kuhamisha zile hisa asilimia 70 zije serikalini na wizara ya fedha, na madini tulikwishakaa ili tuone deni hili tunalilipaje,” amesema Biteko na kuongeza;

“Jumla ya Bil. 40.6 serikali yako ilivyoingia ilikuta hayo madeni yalikuwa hewa, tulipokwenda kuhakiki yalishuka kutoka bili 46 mpaka bil 1.24.

“Wale waliokuwa wanadai, walioletwa serikalini 1,862 baada ya uhakiki walishuka mpaka 862, umefanya kazi kubwa ya kuhakikisha kwamba, tunaondoa madeni hewa.”

Aidha, Biteko amesema, serikali inaendelea na mchakato wa kuhamisha hisa asilimia 70 za Kampuni iliyokuwa inaendesha mgodi huo ya Tan Power Resources, ili kuzirudisha serikalini.

“Wawekezaji wengi wanahitaji kuwekeza, changamoto nyingi ni ile kampuni iliyokuwa inaendesha mgodi ilipotafutwa na Mamlaka ya Mapato (TRA) haikupatikana, ilikimbia.

Naomba nikuhakikishie, tunakamilisha utaratibu wa kuhamisha hisa zile asilimia 70 za kampuni hiyo ili mgodi uanze kufanya kazi haraka,” amesema Biteko.

Mgodi wa Kiwira ulitikisa nchi baada ya (mali hiyo ya umma) kutajwa kumilikiwa na viongozi wa serikali. Hatua hiyo ilisababisha baadhi ya taasisi kuzitenga kwa kukwepa kushiriki kwenye ufisadi.

Miongoni mwao ni Kampuni ya Saruji ya Mbeya ambayo ilisusa kununua nishati hiyo kwa hofu ya kuhusishwa na hujuma na ufisadi dhidi ya mali Watanzania.

Mmoja wa viongozi hao alinukuliwa “tunaamini wananchi ndio wanaohitajika kunufaika na uwekezaji…lakini tunaposikia viongozi waliopata kuongoza serikali wakitajwa kuhusika na ununuzi wenye utata wa mgodi wa Kiwira, tunachelea kuonekana tunaendelea kuunga mkono ufisadi na hujuma dhidi ya mali za walipa kodi.”

Julai 5, 208 aliyekuwa Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro ( CCM) akizungumza na Gazeti la Alasiri alisema, mgodi wa Kiwira ulijengwa na Serikali ya China kwa kwa Dola za Marekani bilioni 4 na kukabidhiwa kwa Serikali ya Tanzania mwaka 1988 na baadaye kuuziwa Bw. Mkapa na Bw. Yona kwa Sh. 700 milioni. Mpaka wakati huo zilikuwa zimelipwa Sh. 70 tu.

Viongozi hao wa serikali walidaiwa kumiliki mgodi huo kupitia kampuni yao ya ANBEM Limited ambayo waliungana na aliyekuwa Yona na wanafamilia wengine kuchukua hisa zake kabla ya kujitoa.

Kampuni zilizotajwa kuwa na hisa sambamba na ANBEN ni pamoja na Kampuni ya DEVCONSULT Limited ambayo ilionesha kuwa ni ya Yona mwenye hisa ya asilimia 90 na mtoto wake Danny Yona mwenye hisa asilimia 10.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Miamka 60 ya Muungano: Tunakwama wapi?

Spread the loveRAIS wa Jamhuri, Samia Suluhu Hasssan, Ijumaa iliyopita, aliongoza mamilioni...

ElimuHabari za Siasa

Serikali kuongeza wanufaika mikopo ya elimu ya juu

Spread the loveSERIKALI imesema itaongeza idadi ya wanufaika wa mikopo ya elimu...

ElimuHabari za Siasa

Serikali kufumua mitaala ya vyuo vikuu, ufundi stadi

Spread the loveSERIKALI inakusudia kufanya mapitio katika mitaala na programu za vyuo...

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

error: Content is protected !!