Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ripoti ya CAG yawaweka njia panda wabunge wa CCM
Habari za SiasaTangulizi

Ripoti ya CAG yawaweka njia panda wabunge wa CCM

Spread the love

BAADHI ya wabunge wa Chama cha Mapinduzi wamedai wapo njia panda, kwani hawajajua kama watachangia ripoti ya Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kutokana na Spika Job Ndugai kuweka azimio kutoshirikiana na mkaguzi huyo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea). 

Wabunge walio wengi ambao hawakutaka majina yao yatajwe wakati wa mahojiano maalum walisema kuwa hawajajua kama watachangia au la.

Wabunge hao kwa nyakati tofauti walisema kuwa hawajaelewa nini kitafanyika ndani ya ukumbi wa bunge wakati wa kujadili ripoti ya CAG ambayo imeishaingia bungeni na imesainiwa na CAG, Prof. Mussa Assad. 

Wabunge hao walisema kuwa wanasibiri maelekezo ya spika na kwa vyovyote vile kutakuwa na maelekezo ni namna gani ya kufanya.

Mmoja wa wabunge wa CCM alisema hali ilivyo kwa sasa pamoja na wingi wa wabunge wa CCM kupitisha azimio lakini ni dalili za uoga.

“Kilichofanyika ni kukurupuka hauwezi kutenganisha Prof. Mussa Assad na CAG sasa ripoti imeletwa bungeni na aliyesahini ni Prof.Assad hapo unaona pamekaaje,” alihoji Mbunge huyo.

Mbunge mwingine alisema kuwa mpaka sasa wabunge hawajajua nini kitafanyika na wanasubiri maelekezo ya Spika.

“Ni kweli ripoti ya CAG amewasilisha ripoti yake kwa Rais na tayari ipo bungeni iliisomwa kwa mbwembe kana kwamba hakuna kitu.

“Lakini mpaka sasa hatujajua kama tutajadili ila nadhani Spika amesafiri nadhani kamati ya maadili na sisi tutakaa katika mkutano wa chama wa wabunge wa CCM (partcoucas) na hapo tutajua cha kufanya,” alisema mbunge huyo.

Naye mbunge wa Mtera Livingiston Lusinde (CCM) alisema kuwa kwa vyovyote vile ripoti itajadiliwa.

“Ripoti itajadiliwa tu kwani kumtenga Prof. Assad na kujadili ripoti ni vitu tofauti ila itafika hatua CAG atachomoka tu,” alisema Lusinde.

Naye mbunge wa Konde Khatibu Said Haji (CUF) alisema kuwa anashukuru bunge kupokea ripoti ya CAG kwani yalikuwa malumbano makubwa kila kona.

Alisema pamoja na kuwepo kwa msemo wa funika kombe mwanaharamu apite lakini kwa ripoti ya CAG litafunikwa kombe ila mwanaharamu hatapita.

Naye mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema) alisema ripoti ya CAG itajadiliwa kwani yeye amefanya kazi yake kadri alivyoweza.

Naye Mbunge wa Mbozi, Frank Mwakajoka (Chadema) alisema ni ajabu kwa wabunge wa CCM kuiogopa ripoti ya CAG.

Alisema kuwa pindi itakapofikia wakati wa kuijadili wabunge watajadili licha ya kuwa bado wabunge hawakajakabidhiwa wabunge ili waanze kuisoma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

error: Content is protected !!