April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Polisi watunukiwa zawadi, wajane wakumbukwa

Spread the love

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limetoa motisha kwa askari wake waliofanya vizuri kwenye majukumu yao ya kulinda wananchi na mali zao. Anandika Mwandishi Wetu … (endelea).

SACP, Lazoro Mambosasa Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda hiyo amesema mpango wa kutoa zawadi kwa jeshi hilo ni mwendelezo wa kuwatia moyo askari wanaopambana na vitendo vya uhalifu na kuhakikisha Dar es Salaam panakuwa mahala salama.

“Zawadi hizi tunazitoa kwa askari wetu wakipambana na vitendo vya kiuhalifu kama tulivyofanya mwaka jana,” amesema.

Ameshukuri Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliyekuwa Mgeni Rasmi wa ghafla hiyo kwa kuwezesha baadhi ya zawadi kwa askari hao.

Amesema kuwa Makonda aliliwezesha jeshi hilo kuwa na programu ya doria ya baiskeri kwa kutoa baiskeri 200 kwa askari.

“Umekuwa karibu sana na sisi kufuatilia mwenendo na hata afya za watendaji wa jeshi la Polisi. Umetusaidia kupata zawadi kutoka kwa wadau mbali kwa ajili ya kuwapa moyo askari wetu ikiwepo mabati na sementi,” amesema Makonda.

Amesema kuwa kwenye zawadi hizo askari 25 wamepewa zawadi pikipiki 25 na mifuko ya saruji 50 kwa askari 13  pia mabati 37.

Amesema kuwa jeshi hilo halijawasahau wanawake wajane ambao waume zao wamefariki kwenye mstari wa mbele wa mapambano dhidi ya uhalifu.

Wajane hao 13 wamepewa Sh. 500,000 kila mmoja sambamba za mifuko ya saruji.

“Wenzetu waliotangulia mbele ya haki wakiwa kwenye mapambano ya kulinda raia na mali zao kwa kuwa mashujaa hao walioacha familia tukaona tuwatunuku wajane wao Sh. 500,000,” amesema Kamanda Mambosasa.

Pia amesema kuwa jeshi hilo limewatunuku zawadi watumishi raia wanaotumikia jeshi hilo watatu ambapo mmoja amepewa pikipiki na wengine mabati 50.

Makonda¬† amewasisitiza: “Wananchi tuwape heshema askari wetu hawa wanafanya kazi nzuri. Sio muda mrefu maeneo ya Mlimani City majambazi walimvamia kijana na kumpiga risasi na hivi karibuni tukisikia panya road, lakini askari hawa walipambana na kumaliza uhalifu huo.”

Amesema kuwa atawasomesha bure watoto wa askari waliofariki kwenye mapambano ya kuwalinda wananchi.

error: Content is protected !!