KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amempigia magoti Rais wa Sudani Kusini, Salvar Kiir akimsihi kiongozi huyo kuachana na mapigano katika taifa lake. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).
Papa Francis amefanya tukio hilo jana tarehe 11 Aprili 2019 alipokutana na Rais Salvar Kiir pamoja na Mpinzani wake Riek Machar, mjini Vatcan.
Kwa mujibu wa video uliyosambazwa katika vyombo vya habari vya kimataifa, inamuonesha Papa Francis akiwabusu miguuni wanasiasa hao, kama ishara ya kuwasihi kuachana na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na kudumisha amani nchini Sudan Kusini.
Salva Kiir aliingia madarakani tangu Sudani Kusini ilipopata uhuru mwaka 2011, kisha mwaka 2013 vita vya wenyewe kwa wenyewe vilizuka nchini humo, vilivyosababishwa na uhasama kati ya Rais Kiir na Machar ambaye alikuwa na mikakati ya kumrithi.
Mnamo mwezi Julai mwaka jana, Rais Kiir aliingia mkataba wa amani na mpinzani wake Riek Machar, ambapo wote kwa pamoja walikubaliana kusitisha mapigano ya wenyewe.
Attachments area
Leave a comment